HUPATI MLO KAMILI? JUA JINSI YA KUJAZIA! | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Monday, December 30, 2013

HUPATI MLO KAMILI? JUA JINSI YA KUJAZIA!


NI kipindi cha kuukaribisha mwaka mpya 2014 na kuuaga 2013. Katika kipindi hiki ni desturi yetu kuwanunulia tuwapendao zawadi na pengine hata kujinunulia wenyewe kama ishara ya kutakiana maisha mema na yenye afya tele.
Kuna zawadi nyingi za kumnunulia umpendae lakini pengine inayoweza kuwa na thamani kubwa na yenye mvuto kwa kipindi hiki ni lishetiba au kwa jina lingine ‘food supplement’ kwa sababu utakuwa umeboresha afya zao baada ya kutumia zawadi hiyo.
Lishetiba zilianza kutengenezwa miaka takribani 50 iliyopita. Hii ilitokana na wanasayansi kubaini kuwa lishe duni ndiyo chanzo cha magonjwa mengi. Wengi waliotumia lishetiba walipona maradhi ya aina mbalimbali.
Mwaka 1994 Baraza la Congress la Marekani liliamua kuweka sheria ya lishetiba (isipokuwa tumbaku na mazao yake) kuwa zitengenezwe, ziuzwe na zitumike chini ya mamlaka na sheria za vyakula.
Pia watengenezaji wa lishetiba walishurutishwa kuweka lebo katika bidhaa zao ikionyesha wazi kuwa si dawa ila ni chakula tu.
Kwa kuwa lishetiba hizo zilizalishwa zaidi ya aina elfu 50, sheria ilitoa maelekezo kuwa lishetiba zote zitumiwe na walaji kupitia mdomoni tu na siyo vinginevyo, awali zilikuwepo mpaka sindano na dripu kama hospitali.
Kadiri dunia inavyoongezeka watu ndivyo fursa ya kupata mlo sahihi inakuwa ngumu na hivyo suala la kujazia upungufu huo kwa kula lishetiba linakuwa ni jambo la lazima.
Kuna aina nyingi za lishetiba, mfano zipo za kuimarisha kinga ya mwili (antioxidant) ambazo zina vitamin C na E, kuna magome ya mkaratusi, juisi ya zabibu ambayo hutoa ahueni kwa wagonjwa wa saratani na wenye maradhi ya moyo, pia imethibitika kuufukuza uzee kwa kufuta makovu na makunyanzi ya uzee huku ikiiacha ngozi iking’ara zaidi na mzee akaonekana kama kijana.
Aidha, zipo lishetiba za ubongo ambazo zimethibitika kuuchachua ubongo wa mlaji na kuimarisha kumbukumbu zake hivyo kuondoa tatizo la  usahaulifu kwa watu wazima na hata wanafunzi. Pia zipo za kuimarisha na kuondoa matatizo kwenye mfumo wa nguvu za uzazi.
Tibalishe zipo za kila aina na kwa kila tatizo, ila hatuwezi kuzitaja zote leo hapa. Tanzania bado ipo nyuma sana katika matumizi ya lishetiba ulinganisha na nchi zingine duniani ambazo zimeweka utaratibu kwa kuuza ‘kila kona’ kuanzia hospitali, maduka ya dawa baridi hadi hotelini na hivyo kufanya upatikanaji wake kuwa rahisi.
Ni ukweli uliowazi kuwa siyo rahisi kupata mlo kamili wenye virutubisho vyote wakati wote, hivyo ni vyema ukajazia upungufu huo kwa kula lishetiba ukiwa na wasaa huo. Sisi kama chombo cha habari tunakuahidi ushirikiano wa dhati katika hili, hivyo usisite kuwasailiana nasi kwa msaada zaidi.
SOURCE:globalpublishers

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers