MJAMZITO AJIFUNGULIA KWENYE KOKOTO | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Sunday, December 29, 2013

MJAMZITO AJIFUNGULIA KWENYE KOKOTO

Stori: Gordon Kalulunga, Mbeya
MASIKINI! Mama mjamzito aliyetambulika kwa jina la Sabina Mwakyusa (28), mkazi wa Kijiji cha Iwala, Kata ya Utengule Usongwe wilayani Mbalizi mkoani hapa anadaiwa kujifungulia nje kwenye kokoto.
INASIKITISHA
Tukio hilo la kufungia mwaka lilijiri nje ya Hospitali Teule ya Ifisi-Mbalizi hivi karibuni na kusababisha masikitiko makubwa kwa mashuhuda waliodai kuwa ishu hiyo ni kali ya kufungia mwaka 2013.
Akizungumzia tukio hilo muda mfupi baada ya kujifungua, Sabina alisema alifika hospitalini hapo Desemba 18, mwaka huu na alipimwa na manesi ambapo walimwambia kuwa hawamuoni mtoto tumboni mwake.
“Baadaye alikuja daktari na kunipima, akaniambia mtoto anaonekana vizuri na ningejifungua mtoto wa kike ndipo nikaendelea kusubiri uchungu zaidi,’’ alisema kwa masikitiko.
UCHUNGU
Alisema ulipofika usiku wa Desemba 19, mwaka huu, alianza kujisikia uchungu, ndipo manesi waliompima mwanzo wakamwambia anatakiwa apimwe tena, jambo ambalo alikataa kwa madai kuwa alikuwa akiumia.
Alidai alipokataa kupimwa ndipo wakamwambia aondoke hospitalini hapo kwa sababu ana kiburi.
KUMBUKUMBU MBAYA
Mama mzazi wa mwanamke huyo, Roda Mwakyusa (50), alisema anaumia akikumbuka yaliyomkuta mwanaye ikiwa ni uzao wake wa kwanza.
Alidai walipotoka wodini huku mwanaye uchungu ukimzidi, walifika getini akazidiwa na kuanza kujifungua ndipo walinzi wa kampuni ya Mult-Lion, wakamsaidia kumpeleka katika upenu wa duka la hospitali hiyo ili kukwepa kokoto zilizopo na mvua iliyokuwa ikinyesha.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya ulinzi, Kinanda Sanga, alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alikiri kwamba lilitokea na wao wakatoa msaada.
Naye wifi wa Sabina, Prisca Nafred, alisema alimpeleka mtoto aliyezaliwa katika hospitali hiyo saa 7:00 mchana wa Desemba 20, kwa ajili ya chanjo, lakini hakupata chanjo kwa madai kuwa alikuwa amechelewa kufika.
Desemba 21, familia hiyo ilimpigia simu mwandishi wetu na kumueleza kuhusu maendeleo mabaya ya mtoto ambapo mwanahabari wetu alitoa taarifa kwa Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto, Mkoa wa Mbeya, Prisca Butuyuyu ambapo makubaliano yalifikiwa kuwa mtoto apelekwe Hospitali ya Rufaa, Kitengo cha Wazazi Meta.
MTOTO ANAENDELEAJE?
Mtoto huyo alipokelewa Meta na kuingizwa kwenye chumba cha joto kisha kuanza kupatiwa matibabu kwa kuwekewa dripu za maji hadi Desemba 23, mwaka huu hali yake ilipotengemaa na sasa anaendelea vizuri.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Louis Chomboko, alipopata taarifa, alichukua hatua ya kwenda kumuona mtoto huyo Meta na kuahidi kulifuatilia suala hilo.
KIKAO
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ifisi Mbalizi, Msafiri Kimaro, Desemba 23, mwaka huu, alipopata taarifa hizo, aliitisha kikao cha wauguzi wanne waliokuwepo siku ya tukio, muuguzi mkuu, muuguzi kitengo cha chanjo.
Alisema wanawake zaidi ya 300 wanajifungulia hapo lakini tukio kama hilo hakumbuki kuwahi kutokea.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers