AIBUUUUU, SHILINGI MILIONI 15 ZAMPONZA MKE WA MTU....SOMA HAPA. | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Thursday, January 23, 2014

AIBUUUUU, SHILINGI MILIONI 15 ZAMPONZA MKE WA MTU....SOMA HAPA.

Stori: Issa Mnally na Richard Bukos
MWANAMKE aliyetajwa kwa jina moja la Winfrida ambaye ni mke wa mtu amekwaa aibu ya karne baada ya kudaiwa kutaka kuuza kiwanja ambacho si mali yake na kujipatia fedha isivyo kihalali kutoka kwa mtu aitwaye Stanlaus Hajj ‘Stan’, Ijumaa lina mkanda kamili.
Winfrida ambaye ni mke wa mtu akiwa mikononi mwa polisi baada ya kunaswa.
Awali ilidaiwa kuwa mwanamke huyo, alichukua Sh. milioni tano kama malipo ya awali alinasa katika mtego wa polisi wa Kituo cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar alipokuwa akifuatilia Sh. milioni 15 ili aweze kuuza kiwanja hicho kwa Sh. milioni 20.
Winfrida akiwa kwenye gari kuelekea kituo cha Mabatini.
Madai hayo yapo katika Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar baada ya mwanamke huyo kuwekewa mtego na kunasa maeneo ya Mlimani City.
Ilielezwa na mashuhuda wetu kwamba mwanamke huyo ambaye ni mkazi wa Bagamoyo, Pwani alinaswa baada ya kuwekewa mtego na polisi alipotaka kuchukua fedha hizo.

...Mtuhumiwa akificha sura yake akiwa kwenye gari kuelekea kituoni.
Akizungumza na waandishi wetu, Stan alisema mwanamke huyo alimwonesha kiwanja maeneo ya Bunju, Dar ambacho alitaka amuuzie kwa Sh. milioni 20.
“Tulienda Bunju akanionesha kiwanja tukakubaliana bei lakini akaniambia nimpatie milioni tano kwanza kwa kuwa alikuwa na shida na ada za watoto wake, tukaandikishiana nikampa,” alidai Stan.
Winfrida akishuka katika gari baada ya kufika kituoni.
Alidai kuwa, baada ya siku mbili alikwenda kukiangalia kiwanja hicho akiwa na rafiki yake aitwaye Kassim Rashid lakini wakashangaa kumkuta mlinzi, walipojieleza wakaambiwa kuwa wametapeliwa.
Alisema kuwa mlinzi huyo aliwaambia kuwa eneo hilo siyo la mwanamke huyo kwani ameshawauzia watu wengi kiwanja hicho na kuwataka waondoke.
...Akielekea kituoni kwa aibu.
“Nilichanganyikiwa lakini rafiki yangu akanipa moyo na ushauri kuwa nikatoe taarifa katika Kituo cha Polisi cha Wazo ambako nilifungua jalada la kesi namba WH/RB/494/2014 -KUJIPATIA PESA KWA UDANGANYIFU,” alisema  Stan.
“Kassim alinishauri nimpigie simu mama yule na kumwambia fedha iliyobakia nitampa baada ya siku tatu ili kumvuta tumkamate kama tulivyofanya leo (Jumanne wiki hii),” alisema.
...Akiingia kituoni.
Baada ya siku tatu, mtego wa kumnasa mwanamke huyo ukapangwa baada ya kumtaka afike kuchukua fedha zake zilizobaki.
Stan na mwanamke huyo walipanga kukutana katika Baa ya Msumbiji ilioyopo maeneo ya Mlimani City ambako Stan alikuwa amejipanga akiwa na polisi wa Kituo cha Kijitonyama (Mabatini).
Winfrida akiwa kituo cha Mabatini, Kijitonyama, Dar.
“Nawashukuru polisi hasa  Mkuu wa Upelelezi, Ezekiel pamoja na Mkuu wa Kituo, Mapunda maana baada ya kuwapa ile RB ya Wazo walinipa ushirikiano mkubwa sana na wakanipa gari na kufanikisha kumtia mbaroni yule mwanamke,” alisema Stan.
Mwanamke huyo alipofika eneo walilopanga kukutana na Stan alinaswa katika mtego huo kisha kusweka rumande Mabatini kusubiri sheria ichukue mkondo wake.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers