AM KWELI HUJAFA HUJAUMBIKA SHUKURU KWA KUPEWA AFYA NZURI, TAZAMA UGONJWA WA AJABU UNAVYOMTAFUNA MTU HUYU | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Tuesday, January 7, 2014

AM KWELI HUJAFA HUJAUMBIKA SHUKURU KWA KUPEWA AFYA NZURI, TAZAMA UGONJWA WA AJABU UNAVYOMTAFUNA MTU HUYU


Wakati mwingine binadamu huwa tunajisahau kumshukuru Mungu kwa afya nzuri aliyotupa bila kujua kuwa wapo watu duniani wanaoteseka mno. Mwanaume huyu wa nchini Indonesia ambaye mwili wake umefunikwa na upele mkubwa ameiomba dunia imsaidie kumponya tatizo lake ambalo sasa limesababishwa ashindwe kuona vizuri baada ya madude hayo kufunika macho yake.
Slamet, anayetokea East Java, anaaminika kuwa na ugonjwa uitwao neurofibromatosis. Kwa mujibu wa kaka yake, Suwadi, ndugu yake huyo mwenye miaka 59 aliondolewa kitu kama jipu kwenye kiuno chake mwaka 1991. Lakini miezi sita baadaye vipele vingine vikaanza kutoka usoni na kwenye mwili wake.
Miaka kadhaa baadaye hali hiyo imekuwa isiyovumilika kwakuwa Slamet husikia maumivu mwilini muda wote. Majipu hayo kwa sasa yamekuwa mengi kiasi cha kuziba pua zake na kumfanya apumue kwa tabu.

Mshukuru Mungu kwa kukupa afya nzuri uliyonayo. Toa shukrani zako kwa kucomment hapa chini..

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers