BAADA YA WASTARA KUSEMA ANATAKA APATE BWANA MWENYE HELA NDEFU..!! MSHABIKI WAMGEUKIA NA HIKI NDICHO WALICHOFUNGUKA. Wastara Juma Issa aliyekuwa mke wa marehem Sajuki ambaye amepata heshima kubwa kwenye tasnia ya uigizaji na Tanzania kiujumla kutokana na kile kinachoonekana kuwa na upendo wa dhati kwa marehemu mume wake kutokana na kitendo chake cha kuwa bega kwa bega na mumewe wakati wote wa raha na hata maradhi yalipokujakumkuta, matibabu na hadi umauti unamkuta hakuwahi kumtenga au kumnyanyapaa kwa chochote.
Kutokana na upendo huo aliouonyesha ambao hakuna mwanaume mwenye akili timamu asiyependa kuwa na mwanamke wa aina hiyo, mara baada ya mumewe kufariki na msiba kupita inasemekana wanaume wengi walianza kumsumbua na hata mara kadhaa kuzushiwa skendo kwamba anatoka na huyu mara yule na maneno mengine mengi. Kwake ilimchukua muda hadi kuja kuongea kwamba yote ni fununu tu na hakuna kitu kama hicho kwake kwa madai kwamba wanaume wengi wanamtamani na si kumpenda kwa dhati.


Hali ya tetesi hizo imeendelea na safari hii kuibuka na headlines kwamba Wastara anatafuta mtu mwenye hela nyingi ili amuoe na sio kuwa na bora mtu tena hohehahe kitu kilichowastua mashabiki wake wengi ambao walipata fursa ya kuzungumza na chanzo chetu kimoja ambapo mbali na kueleza hisi zaoo kwa Wastara lakini pia walitoa ushauri kwa nyota huyo wa filamu Bongo anayetamba na filamu ya Shaymaa iliyopo sokoni kwa sasa.
“Kati ya mastaa tunaowakubali kwa kujiheshimu na kutojihushisha na mambo ya ajabu, Wastara ni miongoni mwao so now tumepigwa butwaa la nguvu kwanini aanze kubadilika, kwanini asijitulize tu agange kwenye kazi yake moja na kukubaliana na kipato alichonacho? Sisi kama fans wake tunamuomba asikariri kwamba kufanikiwa mpaka uhongwe no!! jitihada zake mwenyewe ndizo zitakazomletea mafanikio.”
BAADA YA WASTARA KUSEMA ANATAKA APATE BWANA MWENYE HELA NDEFU..!! MSHABIKI WAMGEUKIA NA HIKI NDICHO WALICHOFUNGUKA. BAADA YA WASTARA KUSEMA ANATAKA APATE BWANA MWENYE HELA NDEFU..!! MSHABIKI WAMGEUKIA NA HIKI NDICHO WALICHOFUNGUKA. Reviewed by Linnah Lsquare on 4:51 AM Rating: 5
Powered by Blogger.