IMETHIBITISHWA KUWA WAZIRI WEA FEDHA Dk. William Augustao Mgimwa AFARIKI DUNIA AFRIKA KUSINI..SOMA ZAIDI HAPA... | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Wednesday, January 1, 2014

IMETHIBITISHWA KUWA WAZIRI WEA FEDHA Dk. William Augustao Mgimwa AFARIKI DUNIA AFRIKA KUSINI..SOMA ZAIDI HAPA...Waziri wa Fedha, Dk. William Augustao Mgimwa (63) amefariki dunia.

Taarifa za hivi punde zinasema Waziri huyo wa fedha katika serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete amefariki dunia hii leo baada ya kuugua na kulazwa nchini Afrika Kusini. 

Mgimwa aliyezaliwa January 20, 1950 na kuwa mbunge wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Binafsi ya Milpark ya nchini humo. 

Dk. Mgimwa alikuwa mkufunzi katika Chuo cha Benki mkoani Mwanza, kabla ya kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Mkoa wa Iringa, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Hospitali hiyo ya Milpark ndiyo imekuwa ikitumiwa na Serikali ya Tanzania kupeleka watu wanaoumwa na mtu wa karibuni zaidi kuhudumiwa katika hospitali hiyo ni marehemu Dk. Sengondo Mvungi.

Tutawapa taarifa kamili ya Msiba huo mkubwa wakati wowote kuanzia sasa.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers