DUH!....TAZAMA MASOGANGE AKIKATA MAUNOVideo Queen Agnes Jerald ‘Masogange’akikata mauno.
Stori: Imelda Mtema
BAADA ya kujificha muda mrefu tangu atoke mahabusu nchini Afrika Kusini kwa msala wa madawa ya kulevya, Video Queen Agnes Jerald ‘Masogange’ amenaswa ‘live’ akikata mauno huku akipewa kampani na mtoto mdogo nyuma yake.


Agnes Jerald ‘Masogange’ akiwa nyumbani kwa Salma Jabu ‘Nisha’, Kijitonyama jijini Dar
Weekly Star Exclusive  ilimbamba mrembo huyo juzikati nyumbani kwa mwigizaji Salma Jabu ‘Nisha’, Kijitonyama jijini Dar ambapo Nisha alikuwa akipiga makofi na kushangilia wakati Masogange alipokuwa akikata mauno.
“Sijacheza siku nyingi jamani ndiyo maana leo nimejikumbushia mambo yangu ya mjini, kuna vitu vingi sana nilivimisi kama kukutana na watu hivi na kucheka pamoja kwa uhuru,” alisema Masogange.
Wakati akiendelea kukatika, mtoto mdogo ambaye jina lake halikupatikana mara moja mwenye umri uliokadiriwa kama miaka 7, alishangilia na kucheza naye pamoja.
Tangu arejee kutoka Bondeni, Masogange amekuwa shosti mkubwa wa Nisha ambapo mbali na urafiki, wanafanya filamu pamoja iitwayo Betina na Zena.
Kwenye msala wa madawa ya kulevya, Masogange aliachiwa kwa kulipa faini baada ya kuthibitika kuwa mzigo aliokutwa nao haukuwa madawa ya kulevya bali ni ‘material’ ya kutengenezea madawa tofauti.
DUH!....TAZAMA MASOGANGE AKIKATA MAUNO DUH!....TAZAMA MASOGANGE  AKIKATA MAUNO Reviewed by Linnah Lsquare on 11:05 PM Rating: 5
Powered by Blogger.