"HAKUNA MWANAMKE YEYOTE MWENYE UBAVU WA KUMCHUKUA BWANA'ANGU KWANI ME NI ZAIDI YA HAO WOTE" IRENE PAUL | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Monday, January 20, 2014

"HAKUNA MWANAMKE YEYOTE MWENYE UBAVU WA KUMCHUKUA BWANA'ANGU KWANI ME NI ZAIDI YA HAO WOTE" IRENE PAUL


MSANII nyota wa filamu Irene Paul, amesema kwamba haoni mwanamke mwenye uwezo wa kumuibia bwanaake, ingawa hataki kumtaja hadharani kwakuwa alishaapa kutoyaanika maisha yake binafsi hata kabla hajawa staa.

Irene alizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni ambapo alisema kwamba mashabiki wake wanatakiwa kujua kwamba anampenzi .
"Mtu anataka niweke hadharani bwana wangu wakimjua watapata nini??
Hakuna anayeweza kumchukua mpenzi wangu hilo najua lakini masiha yangu ya sanaa tofauti na yale binafsi hivyo mashabiki wangu naomba wafahamu hilo", alisema.

Hata hivyo alisema kwamba amekuwa mtu wa kuheshimu mambo yake ya ndani kwani ndiyo yanaweza kuharibu kila kitu endapo atafanya matangazo kama wengine wanavyofanya.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers