HAYA NDIYO MADHARA YA WIZI!! APIGWA RISASI WAKATI AKIJARIBU KUIBA KWENYE KITUO CHA GESI | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Saturday, January 25, 2014

HAYA NDIYO MADHARA YA WIZI!! APIGWA RISASI WAKATI AKIJARIBU KUIBA KWENYE KITUO CHA GESI

Tukio la kustaajabisha limetokea hapo jana mchana nchini Brazil,ambapo vijana wawili walijikuta hatiani baada ya mmoja wao kupigwa risasi wakati wakijaribu kuiba katika kituo cha gesi. Vijana hao wakati wakujaribu kutoroka kutoka katika eneo la tukio walijikuta wakikumbwa na dhahama hiyo baada ya mtu mmoja aliyekuwa jirani na kituo hicho cha gesi alimpiga risasi ya mgongo mmoja wa vijana  hao.Hata hivyo  vijana  hao walifanikiwa kupanda pikipiki na kukimbia,lakini baadae mmoja wao alianguka umbali mchache kutoka eneo la tukio na kufa hapohapo.

Mwizi mwenzake aliyekuwa nae,alifanya tukio lililoshangaza watu wote eneo hilo,alivyoona mwenzake amezidiwa alisimamisha pikipiki na kumshusha,bila yeye kujulikana alipoelekea.


Polisi bado wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hili,ingawa taarifa za awali za jeshi la Polisi nchini humo zinasema wawili hao ni miongoni mwa wahalifu sugu wanaotafutwa kutokana na wizi wa aina hiyo katika maeneo tofauti ya nchi hiyo.
Kiongozi wa Polisi nchini humo alibeza tukio la wezi hao kama alivyonukuliwa akisema 'I just love seeing the people getting fed up with crime and doing the police and judicial system’s job. No tax money to feed this moron in prison. I would throw his body in a sewer and present the rats with a late Christmas present'.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers