HAYA SASA LILE KANISA LA WALA NYASI, WENGI WATAKA KUJIUNGA | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Monday, January 20, 2014

HAYA SASA LILE KANISA LA WALA NYASI, WENGI WATAKA KUJIUNGA


Na Mwandishi Wetu
BAADHI ya wananchi jijini Dar wamejitokeza na kuomba kujiunga na kanisa ambalo waumini wake wanakula nyasi.
Waumini wakila nyasi.
Kanisa hilo ambalo makao yake makuu ni Afrika Kusini linaloitwa Rabboni Centre Ministries gazeti hili liliandika katika toleo lake lililopita kuwa limeingia nchini na lipo maeneo ya Upanga jijini Dar.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili mara baada ya kusoma habari hiyo walisema wanatamani kujiunga.
“Mimi nataka kujiunga na kanisa hilo kwa sababu tunataka wokovu,” alisema mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Amos.
Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Frida Mandade alisema ana hamu ya kujiunga na kanisa hilo kwa sababu zake binafsi.
Kanisa la Rabboni Centre Ministries lina makao yake makuu Pretoria nchini Afrika Kusini na linaongozwa na mtu anayejiita Mchungaji na Nabii Daniel Lesego ambaye alilianisha mwaka 2002.
Wakati wa mfungo waumini wa kanisa hilo wametajwa kuwa huwa wanaishia kula majani yaliyopo nje ya kanisa hilo kwa imani kuwa Roho Mtakatifu huongoza mtu kula chochote manyasi hayo ni chakula kutoka mbinguni.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers