JOYCE KIRIA AFICHUA SIRI YA NDOA ZAKE
Ndoa ya pili ya Joyce Kiria na Henry Kilewo.
Na Mwandishi Wetu
MTANGAZAJI wa Runinga ya Channel 5, Joyce Kiria amefunguka na kufichua siri ya ndoa zake mbili alizofunga, Risasi Mchanganyiko lina habari kamili.
Ndoa ya kwanza ya Joyce na DJ Nelly.
Kwa mujibu wa mtandoa mmoja wa kijamii, Joyce alisema kwamba ndoa yake ya kwanza aliyofunga na Nelson Nkongo ‘DJ Nelly’ walichangisha watu ili kufanikisha ndoa hiyo.
“Kama desturi na utamaduni wetu tulichangisha lakini pamoja na michango mingi, tuliingia gharama zetu na kama haitoshi tulikopa na baada ya shughuli tulianza kupiga miayo ya njaa, hatukuwa na fedha tena na madeni yakatuandama,” alisema Joyce.

Joyce na Kilewo siku ya ndoa yao.
Mtangazaji huyo wa Kipindi cha Wanawake Live alisema kwamba alijuta sana lakini ikafika hatua ndoa hiyo ikasambaratika.
Akiizungumzia ndoa yake ya pili na Henry Kilewo, ambayo awali ilifungwa Bomani, Joyce alisema kwamba haikuwa na makeke na wala kuchangisha watu fedha.

Kilewo akimvisha pete Joyce.
“Henry aliandaa sherehe ndogo sana, ndugu jamaa na marafiki wachache walihudhuria, hatukumsumbua mtu yeyote. Baada ya lile tukio wala hatukupata ile adha ya madeni na kuishiwa pesa kabisa, tukaendelea na maisha matamu kwa upendo na uaminifu mpaka sasa,” alisema.
Joyce Kiria.
Joyce ambaye hivi karibuni alibariki ndoa yake na mumewe kanisani alisema kama angekuwa na mawazo mgando angefanya sherehe ya kukata na shoka kutetea umaarufu wake na kuwazodoa waliomwambia kwamba kanisa angelisikia kwenye runinga, redio na magazeti.
Joyce katika vazi la harusi.
“Wengi wanafanya sherehe kubwa ili kuwakoga au kuwafurahisha watu wengine kutokana na kudanganyika na majina yao na kuwafanya wajitutumue kuliko uwezo walionao,” alisema.

JOYCE KIRIA AFICHUA SIRI YA NDOA ZAKE JOYCE KIRIA AFICHUA SIRI YA NDOA ZAKE Reviewed by Linnah Lsquare on 1:05 AM Rating: 5
Powered by Blogger.