KAJALA ALEWA TILALILA, AGEUKA KITUKO.....MTAZAME HAPA! | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Monday, January 20, 2014

KAJALA ALEWA TILALILA, AGEUKA KITUKO.....MTAZAME HAPA!

Stori:  IMELDA MTEMA
STAA wa sinema za nyumbani (Swahili Hood), Kajala Masanja amegeuka kituko nyumbani kwa Wema Isaac Sepetu, Kijitonyama, Dar baada ya kulewa tilalila na kuwaacha midomo wazi wasanii wenzake, Ijumaa Wikienda lina kisa na mkasa.
Kajala Masanja.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, Kajala alifanya madudu hayo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akirekodi filamu yake inayokwenda kwa jina la Laana ambapo waigizaji wenzake walikuwa nje wakisubiri atoke aanze ‘kushuti’ kumbe alikuwa kaegemea mlango huku akiangua kicheko bila kujua afanye nini.

Ilisemekana kuwa baada ya maji kuzidi unga, mwongozaji wa filamu hiyo, Leah Ndemesamkye ‘Lamata” ilibidi ashikwe na kigugumizi baada ya kuona mauzauza hayo ya Kajala na kumuuliza ni kitu gani ambacho kimempata kwani kila anachoongea naye, yeye anaishia kucheka mfululizo.
Baada ya gazeti hili kupata habari hizo lilimvutia waya Kajala ili kudhibitisha madai hayo ambapo Kajala alikiri kulewa kidogo na kumtupia mpira rafiki yake kipenzi Wema kuwa ndiye aliyemnywesha.
Alisema: “Unajua nini, siku hiyo tulilala kwa Wema, ndiye aliyeninywesha pombe lakini mbona kazi iliendelea kama kawaida jamani?”

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers