Kapombe apanda ndege kwenda Ufaransa, ashushwa Nairobi, arudishwa Dar | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Thursday, January 23, 2014

Kapombe apanda ndege kwenda Ufaransa, ashushwa Nairobi, arudishwa Dar

Shomari Kapombe.
Khadija Mngwai na Nicodemus Jonas
SAKATA la Shomari Kapombe kukwama kwenda nchini Ufaransa alipokuwa akicheza soka la kulipwa linaashiria hali ni tete zaidi.
Imeelezwa kuwa Kapombe ambaye alirejea nchini kuitumikia Taifa Stars, Desemba, mwaka jana, kisha kukwama kurudi Ufaransa, alipanda ndege kwa ajili ya kuelekea nchini humo lakini alipofika Nairobi nchini Kenya, akashushwa, kisha akarejeshwa Tanzania.
Safari ya Kapombe ilikuwa ni kurejea kwenye klabu yake ya AS Cannes inayoshiriki Ligi Daraja la Nne Ufaransa lakini kutokana na visa yake kuwa na matatizo, akalazimika kuishia Nairobi na kurudi jijini Dar es Salaam ambako ndiko alipo mpaka sasa.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema baada ya wao kumfanyia mipango yote ya kusafiri kwenda Ufaransa, safari ikaanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar.
“Mara ya kwanza alichelewa ndege, hivyo tukaamua kumkatia nyingine, ambapo alipofika Nairobi alikwama kwa muda kutokana na visa yake kuonekana ina matatizo, ikabidi arudi huku (Dar) ambapo ikabidi tumfanyie tena mipango na tukamwekea kila kitu sawa.
“Baada ya kukamilisha, tunashangaa hajaondoka tena, kwa hiyo upande wetu sisi hatujui kinachoendelea na wala hatuna njia nyingine ya kumsaidia, kama ni suala la madai basi ni juu ya wakala wake, ndiye anayejua na ndiye anayetakiwa kufuatilia kila kitu.
“Kapombe alikuwa na nafasi nzuri kuweza kucheza na kufanikiwa kusonga mbele zaidi kisoka tofauti na hapa nchini lakini mwenyewe ndiye mwenye maamuzi na kile kilichotokea na anajua nini kinaendelea,” alisema Wambura.
Akizungumzia suala la Kapombe, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema: “Nazionya klabu nyingine ambazo zinamrubuni kwa kuwa zitajiingiza kwenye matatizo.
“Kapombe tayari ameshalipwa fedha zake, euro 2,000 alizokuwa akiidai Klabu ya AS Cannes na Simba itamsafirisha kurejea Ufaransa, kufikia Jumatatu ijayo (Januari 27) atakuwa ameshaondoka kwenda Ufaransa.”

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers