MAMLAKA YA HEWA NCHINI YAKANUSHA KUHUSIKA NA UJUMBE HUU SOMA HAPA. | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Tuesday, January 14, 2014

MAMLAKA YA HEWA NCHINI YAKANUSHA KUHUSIKA NA UJUMBE HUU SOMA HAPA.

Kuna taarifa inayosambazwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi (SMS) kuhusiana na TMA kutoa tahadhari ya Tsunami


Taarifa hizo sio za kweli, uionapo ujumbe huu upuuzie kwa kuwa sio taarifa sahii, ni taarifa ya upotishaji


Kuna taarifa inayosambazwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi (SMS) kuhusiana na TMA kutoa tahadhari ya Tsunami


Taarifa hizo sio za kweli, uionapo ujumbe huu upuuzie kwa kuwa sio taarifa sahii, ni taarifa ya upotishajiTaarifa rasmi ni kama ilivyotolewa awali kuhusiana na upepo mkali kwa Ukanda wa Bahari ya Hindi na Mvua kubwa.
Ujumbe huo unasomeka kama hivi:


"TAHADHARI ya Tsunami: Kuanzia saa moja usiku Tsunami itafika Tanzania na mawimbi yatakuwa makubwa kuanzia muda huo. Taarifa zaidi itatolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wakati wowote kuanzia sasa, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agness Kijazi."

Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa ili kutoa taarifa sahihi ni vizuri kuwasiliana na Ofisi zetu kwa maelezo ya kina zaidi kuepusha mkangamanyo kwa wananchi


Asante tena kwa ushirikiano wako,


Nakutakia Sikukuu njema ya Maulid,


Monica Mutoni


Ofisi ya Uhusiano


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers