MAYA ASAKAMWA MADAI YA RUSHWA, AONGEA

Na Mwandishi Wetu
BAADA ya kuzagaa kwa habari kuwa viongozi wa kamati ya uchaguzi wa Klabu ya Bongo Movie wamebwia rushwa, Mayasa Mrisho ‘Maya’ ameibuka na kukanusha taarifa hizo.

Mayasa Mrisho ‘Maya’.
Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar na kumtangaza Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ kushinda nafasi ya uenyekiti, baadhi ya wasanii waliibua minong’ono kuwa kamati ya uchaguzi ‘ilipozwa’ ili kupindisha matokeo.
“Hatukuchukua rushwa kutoka kwa mtu yeyote, uchanguzi ulikwenda vizuri na kila kitu kipo katika rekodi, anayetaka kuonyeshwa mfumo mzima wa kura atuone,” alisema Maya.
MAYA ASAKAMWA MADAI YA RUSHWA, AONGEA MAYA ASAKAMWA MADAI YA RUSHWA, AONGEA Reviewed by Linnah Lsquare on 11:58 PM Rating: 5
Powered by Blogger.