MBOTO: SIJAWAHI KUTOKA NA AUNT EZEKIEL | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Sunday, January 12, 2014

MBOTO: SIJAWAHI KUTOKA NA AUNT EZEKIEL

KAMA kawa, kama dawa, wiki iliyopita tulimleta kwenu ‘komediani’ kiraka Bongo, Haji Salum almaarufu Mboto ambaye mulimuuliza maswali magumu ambayo wiki hii anayajibu na kuchambua moja baada ya lingine. UNGANA NAYE…
ATAOA LINI?
Mboto wewe ni mchekeshaji mahiri kunako kiwanda cha maigizo Bongo, je, unategemea kuoa lini? Salim Liundi, Dar, 0658110395
MBOTO: Asante, suala la kuoa siyo la kukurupuka kwa hiyo inahitaji utulivu na kuoa kwangu siyo leo wala kesho.
FILAMU
Hivi Mboto ulishawahi kutoa filamu yako mwenyewe na kama umewahi kutoa inaitwaje? Kama hujawahi kutoa tatizo ni nini? Muddy Madiley, 0652672805
MBOTO: Nimefanya filamu yangu inaitwa Bana Kongo nimeigiza kama Mkongomani lakini bado haijatoka, inatarajiwa kutoka ndani ya mwezi huu.
USHAURI
Haina ubishi una kipaji kikubwa katika uigizaji ila nakukumbusha usimsahau Mungu kwani ndiye kila kitu na ambaye amekuwezesha kufika hapo ulipo. Amiri Salumu, Dar, 0653252416
MBOTO: Asante ila mimi ninamwamini sana Mungu na kabla sijaanza kufanya kazi lazima nimuombe Mungu kwanza.
TAHADHARI
Mboto upo juu sana, mimi binafsi nakukubali mzee, kikubwa jitahidi usije ukawa na skendo. Pia muangalie Kinyambe (mchekeshaji) anakuja juu sana. Msomaji, 0716089050
MBOTO: Nashukuru, ni kweli na siyo Kinyambe tu kuna wasanii chipukizi wengi wanaokuja kwa kasi lakini mimi ninaendelea kupigana zaidi ili niendelee kufanya vizuri.
PONGEZI
Kaka Mboto nakukubali sana kunako gemu la uigizaji kama Filamu ya Kibajaji, hongera ila ningependa kujua umeoa na una watoto wangapi? Naika, Dar, 0657433268
MBOTO: Bado sijaoa ila nina mtoto mmoja.
Aunt Ezekiel.
AUNT EZEKIEL?
Mboto nafurahi sana kila nikikuona. Je, wewe ni Mpemba kweli? Je, ni kweli ulishawahi kutoka kimapenzi na Aunt Ezekiel? Sarha, Dar, 0653358681
MBOTO: Mimi siyo Mpemba bali ni Mzaramo wa Mtanga, sijawahi kutoka na Aunt Ezekiel na sijawahi kufikiria kwa sababu tumeshakuwa kama ndugu yeye ananiita kaka na mimi namuita dada.
NJE YA FANI
Nje na fani ya uchekeshaji unajishughulisha na kazi gani nyingine? Msomaji, 0755708366
MBOTO: Mimi ni mfanyabiashara
HISTORIA
Nakukubali sana Mboto, ningependa kujua historia yako japo kwa kifupi. Bahati, Mbeya, 0753280224
MBOTO: Nimezaliwa Temeke na kusoma hukohuko, sanaa nimeanza nikiwa sekondari na nilijiunga rasmi na Kundi la Kaole Sanaa mwaka 1999.
Baada ya hapo nikiwa na wasanii wengine tuliunda kundi letu lililoitwa Katavi ambalo tulitengeneza mchezo wa kwanza uliokuwa ukirushwa na Runinga ya ITV ulioitwa Jabali. Pia tulitengeneza Tamthiliya ya Tunduni iliyokuwa ikirushwa na Star TV.  Baada ya michezo hiyo ndipo nikaingia kwenye filamu mpaka sasa.
MIPANGO
Kaka Mboto wewe ni mahiri na mchekeshaji bora wa filamu, je, una mipango gani hapo baadaye katika filamu? Stella Maeda, Dar, 0653648869
MBOTO: Nina mpango wa kuanzisha kampuni yangu ya filamu nifanye kazi na wasanii chipukizi.
ANAJISIKIAJE?
Mboto wewe ni msanii mkubwa uko juu sana katika sanaa ya uigizaji  hongera kwa hilo, unajisikiaje pale unapocheza muvi na Aunt Ezekiel na Monalisa? Msomaji, 0652952688
MBOTO: Huwa najisikia faraja sana kwa sababu ni watu ambao wanaielewa sanaa hawana nyodo, hakuna kuwaelekeza sana tofauti na wengine ambao wana majina makubwa lakini unawaelekeza mpaka unachoka.
MAFANIKIO
Mboto ni mafanikio gani umepata tangu ulipoanza sanaa? Fredy, 0786930888
MBOTO: Nimejuana na watu wengi na kuwa na marafiki wengi ambao wamenipa ushauri kama hivi ninafanya biashara na miradi ambayo sitaki kuiweka wazi kwa sasa.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers