MCHAWI APATIKANA BAADA YA KUANGUKA NA UNGO AKIWA SAFARINI HUKO SHINYANGA...JIONEE PICHAZ HAPA...


Kikongwe mwenye umri kati ya miaka 85 hadi 90 ambaye bado hajafahamika jina lake amekutwa katika kijiji cha Nyashimbi kata ya Muhongolo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kwa kile kinachodaiwa kuwa huenda ni mchawi aliyeanguka usiku wakati akiwa kwenye safari zake angani.

Kwa mujibu wa wakaazi wa Kijiji hicho bibi huyo ameonekana leo majira ya saa 12 asubuhi akiwa katika vichaka vilivyo kando ya barabara na alipoulizwa aliongea kidogo tu kuwa anatoka Kijiji cha Nyihogo wilayani Kahama.

Kikongwe huyo akiwa chini huku amezingirwa na kundi la wananchi

Akiwa amelala chini kwa kile kinachodaiwa ni njaa

Alipoendelea kuhojiwa alisema alikuwa na wenzake na vitu mbalimbali ila wamemuacha, huku akisema hawezi kuongea zaidi kwani anahisi njaa kwakuwa alikula toka jana tena chakula Kibichi, jibu ambalo liliwashangaza wengi ni aina gani ya chakula ambacho huliwa kikiwa kibichi. 
Bibi huyo amekutwa na nguo moja ya Kimasai na nguo zingine chache za kawaida lakini hakukutwa na vitu vyovyote vinavyoashiria kuwa huenda ni mchawi, hivyo kuleta hisia kuwa huenda alikuwa ni mtembea kwa miguu tu aliyepotea njia kwani watu wote wa eneo hilo hakuna anayemtambua.


Wananchi wakimwangalia bibi kizee huyo akiwa hio bin taaban


Bibi kizee huyo akiwa ameanguka chini usiku wa kuamkia leo
 


MCHAWI APATIKANA BAADA YA KUANGUKA NA UNGO AKIWA SAFARINI HUKO SHINYANGA...JIONEE PICHAZ HAPA... MCHAWI APATIKANA BAADA YA KUANGUKA NA UNGO AKIWA SAFARINI HUKO SHINYANGA...JIONEE PICHAZ HAPA... Reviewed by Linnah Lsquare on 11:36 PM Rating: 5
Powered by Blogger.