NJAA YAWAKIMBIZA MJI MSANII JACK PENTEZEL NA MUMEWE WADAIWA KUSHINDWA KULIPA KODI YA NYUMBA MJINI...!!!Muigizaji wa filamu za kibongo nchini Jacqueline Pentezel na mumuwe, Gadner Dibibi  wamedaiwa kuukimbia mji  kufuatia kukutwa na  ukata uliowafanya washindwe kumudu gharama za kuishi Mwananyamala Koma Koma na badala yake kuelekea nje ya jiji.

Habari kutoka kwa chanzo cha uhakika, kilicho ndani ya familia ya muigizaji huyo zilisema; “Kaka habari ndiyo hiyo, siyo siri, ndugu yetu maisha yamemshinda, amekimbia mji sasa hivi yuko huko sehemu moja huko Mbezi kavu, ndani ndani hata kama ukielekezwa unaweza kuchukua siku mbili hadi kufika nyumbani kwake,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilisema sababu kubwa ya wawili hao kuliacha jiji, ni baada ya kuponda maisha kwa kutumia gharama kubwa bila kujali kwamba walikuwa wakiishi nyumba ya kupanga na kwamba ipo siku kodi itaisha.

“Ndugu yetu alikuwa anaendekeza bata sana, yaani  wao ilikuwa bata banati, basi ndiyo hivyo tena, kwa sasa wanaishi huko nje ya mji kabisa,” alisema msichana huyo.

Maskani Bongo lilivuta waya ili kumpata Jack ambaye kwa bahati nzuri alipatikana na kushuka nah ii hapa.

“ Wewe hao wanaosema mimi nimeshindwa maisha ni wanafiki, na waongo mimi nimehama huko uswahili kwa vile nilikuwa naishi chumba kimoja, lakini huku naishi kwenye nyumba nzima na choo ndani, sasa hapo pima mwenyewe, kama mimi na mume wangu tumefulia au tumepiga bao,” alisema Jack huku akihema harakaharaka kwa hasira 

Hata hivyo, Jack alishindwa kuvumilia, kwani muda mfupi baadaye alipiga tena simu kwa mwandishi wetu na kusema;

“Wewe nakwambia  waeleze hao wanafiki wenzako, mnabakia kufatilia maisha ya watu kuwa mimi sijafulia hata kidogo, nipo huku hata kama ni porini wanavyokwambia, lakini naishi kwa uhuru mkubwa na nyumba nzima,” alisema msanii huyo akimalizia kwa tusi."
NJAA YAWAKIMBIZA MJI MSANII JACK PENTEZEL NA MUMEWE WADAIWA KUSHINDWA KULIPA KODI YA NYUMBA MJINI...!!! NJAA YAWAKIMBIZA MJI MSANII JACK PENTEZEL NA MUMEWE WADAIWA KUSHINDWA KULIPA KODI YA NYUMBA MJINI...!!! Reviewed by Linnah Lsquare on 10:15 AM Rating: 5
Powered by Blogger.