PICHA.... AJALI YA LEO ILIYOUA WANAFUNZI WANNE NA KUJERUHI WENGINE 20 MTWARA! | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Wednesday, January 22, 2014

PICHA.... AJALI YA LEO ILIYOUA WANAFUNZI WANNE NA KUJERUHI WENGINE 20 MTWARA!

WANAFUNZI WATANO WAFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA GARI WAKATI WAKIKIMBIA MCHAKAMCHAKA HUKO MTWARA.
Wanafunzi wanne Wa shule ya sekondari Mustapha Sabodo mjini Mtwara wamekufa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa Vibaya baada ya kugongwa na gari aina ya Benz wakiwa kwenye mchakamchaka asubuhi ya leo.Wanafunzi watano  mkoani Mtwara shule ya sekondari Mustapha Sabodo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Vijijini katika kijiji cha Msijute wamepoteza maisha  baada ya kugongwa na gari aina ya mercedenz benzi no T174 AED km 1 kutoka shule hiyo wakati walipokuwa wanakimbia mchaka mchaka.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Zeloth Stephen akizungumza na waandishi wa Habari  waandishi wa habari, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea asubuhi ya jana (leo jumatano) majira ya saa 11:40 maeneo ya shule hiyo barabara kuu ya Mtwara Lindi  iliyosababishwa na gari lililokuwa likiendeshwa na Baraka Mgwegwe (50) iliyokuwa ikitokea  manispaa y Mtwara Mkindani kuelekea Lindi.
Kamanda alisema  kuwa ajali hiyo imesababisha vifo vya watu wa tano, majeruhi 21 na waliotibiwa na kuruhusiwa katika hospitali ya rufaa ya Ligula ni 26 na kuwataka wananchi kuendelea kuwa na utulivu katika kuwahudumia waliopata madhara na waliotamgulia mbele ya haki.
“Asubuhi ya leo majira ya  saa 11:40 ajali mbaya sana imetokea maeneo ya shule ya sekondari ya Mustapha Sabodo kijiji cha Msijute barabara kuu ya Mtwara- Lindi na polisi wakati huo walikuwa tayari wako kazini na kuweza kutoa huduma ikiwa ni pamoja na kuwaleta hospitali,” alisema Kamanda
Kadhalika, kamanda alisema kwamba mtuhumiwa tayari yuko mbaroni kwa ajili ya kuchukuliwa hatua ambazo ni stahiki.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya Wilman Ndile alieleza kuwa ajali hiyo ni yakusikitisha sana kwa kushirikiana na viongozi wa idara mbali mbali ikiwemo idara ya elimu wameunda kamati ikiongozwa na mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya Ligula pamoja na Afisa elimu wa wilaya ya Mtwara vijiji ili kuona namna gani watasafirisha maiti.
“ Ajali imesikitisha sana imetokea leo  asubuhi tumeweza kufika na kuanza  kushirikiana kama viongozi  na tumeunda kamati ikiongozwa mganga mkuu wa hospitalin ya rufaa ya ligula kuona namna gani  tutasafirisha maiti,” alisema Ndile
Naye Mganga mkuu wa hospitali rufaa ya Ligula,DK. Shaibu Maarifa alikiri kupokea majeruhi na maiti zilizo  tokana na ajali hiyo na kutoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za barabarani na kutoa pole kwa waliofikwa na mkasa huo.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers