ROHO WA KIFO BADO INAWAANDAMA MASTAA | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Friday, January 3, 2014

ROHO WA KIFO BADO INAWAANDAMA MASTAA


Stori: Hamida Hassan na  Haroun Sanchawa
MTOTO wa  aliyekuwa mtabiri  maarufu nchini, Shehe Yahya Hussein, Maalim Hussein Yahya ametoa utabiri wake wa mwaka na kusema kwamba vifo zaidi vitaendelea kutokea kwa mastaa wa filamu, muziki, waandishi wa habari, viongozi wa dini pamoja na wanasiasa, Risasi Jumamosi linaweka bayana.
Aliyekuwa mtabiri  maarufu nchini, Shehe Yahya Hussein.
Akifafanua kuhusu utabiri wake huo, Maalim Hussein alisema kwamba pamoja na vifo hivyo lakini mwaka huu utakuwa ni wa mafanikio kwa baadhi ya mastaa na wanahabari.
Marehemu Ngwea.
“Pamoja na kwamba vifo vitatokea kwa mastaa na wanahabari lakini wapo kati yao watakaopata neema ya uongozi na kuwa watu wakubwa  kwa kushika nyadhifa mbalimbali,” alisema Maalim Hussein.
Akizungumzia kwa upande wa siasa, Maalim Hussein alisema nyota zinaonesha kwamba kuna kiongozi mmoja  kwenye vyama vikubwa vya siasa atavuliwa uongozi ghafla na kutokana na sakata hilo ataanguka na kufariki dunia.
Kama vile haitoshi, Maalim Hussein alisema baadhi ya  viongozi wa dini watapata kashfa ambazo zitawasababishia umauti pamoja kuvuliwa uongozi katika nyadhifa walizonazo.
Maalim huyo ameongeza katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajiwa kufanyika mwaka huu kutatokea vuguvugu kubwa litakalosababisha mapigano ya jamii kwa jamii na jambo hilo huenda likasababisha vifo.
Mbali na misiba hiyo, Maalim Husseina alisema kwamba mwaka huu kutakuwa na msiba utakaoligusa taifa moja kwa moja na kuongeza kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete atafanya tukio kubwa la kutikisa nchi ambalo litaleta neema kubwa kwa jamii.
“Huu ni utabiri wangu kwa mwaka, natarajia kufanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza mengi kwani haya ni baadhi ya  mambo machache kati  ya mengi,” alisema Maalim Hussein.
Mwaka jana, Maalim Hussein alitabiri kutokea vifo vya baadhi ya  mastaa ambavyo vilitokea na kuufanya utabiri wake kutimia

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers