Simba yampiga pini kapombe | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Tuesday, January 21, 2014

Simba yampiga pini kapombeShomari Salum Kapombe.
Na Mwandishi Wetu
TAARIFA za beki Shomari Kapombe kufanya mazungumzo na Yanga na Azam FC zimetibua mambo na Simba imeamua kuanika mkataba wake.
Klabu ya AS Cannes ya Ufaransa ambayo Kapombe anaichezea, ilisema imepata taarifa za mchezaji huyo kufanya mazungumzo na Yanga na Azam FC na wakala wake, Denis Kadito anayeishi nchini Uholanzi akalithibitisha hilo.
Lakini uchunguzi wa Championi Jumatano unaonyesha Kapombe hana uwezo wa kwenda Yanga bila ya klabu hiyo kukubaliana na AS Cannes pamoja na Simba ambao ndiyo wamiliki wa mchezaji huyo.
“Kwanza tumeamua Kapombe aanze mazoezi Simba wakati akiwa hapa nyumbani Tanzania, lakini kama AS Cannes itashindwa kumuuza ndani ya miaka miwili, mkataba unasema anarudi kuichezea Simba na si vingine.
“Kama Yanga wanamtaka basi wajue wanatakiwa kutoa fedha si za kitoto ili tugawane na AS Cannes, kama wakishindwa anarudi Simba ingawa mkataba unasema anatakiwa kulipwa dola 50,000 (zaidi ya Sh milioni 80) za kurudi na mshahara wa zaidi ya dola 2,000 (zaidi ya Sh milioni 3.2),” kilieleza chanzo kutoka ndani ya Simba.

“Mkataba wetu na AS Cannes unasema wakishindwa kumuuza anakuwa mali ya Simba, wakimuuza basi mgawo unakuwa wetu sote. Na kama akivunja mkataba na AS Cannes automatically anarudi Simba, hatuna wasi kabisa na Yanga.”
Kapombe amebaki hapa nchini ikiwa ni kususa kutokana na kutolipwa mshahara wake wa mwezi mmoja ingawa AS Cannes walidai TFF wanapaswa kumlipa kwa kuwa walimchelewesha kurudi Ufaransa alipokuja kuichezea Taifa Stars.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers