TASWIRA ZA KIKAO CHA RIPOTI YA CAG KILICHOPELEKEA MEYA WA BUKOBA ANATORY AMANI KUJIUZULU | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Friday, January 17, 2014

TASWIRA ZA KIKAO CHA RIPOTI YA CAG KILICHOPELEKEA MEYA WA BUKOBA ANATORY AMANI KUJIUZULU

Kutoka kushoto: Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Fabian Massawe, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh wakiingia ukumbini leo mjini Bukoba.
Viongozi hao wakifungua kikao hicho cha kusomwa ripoti ya ukaguzi maalum ya CAG.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila akifungua kikao.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Fabian Massawe akimkaribisha mgeni rasmi leo kwenye kikao hicho cha kukamilisha Ukaguzi Maalum " Exit Meeting" cha CAG.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh akisoma ripoti ya ukaguzi maalum leo Bukoba.
Baadhi ya waliohudhuria kikao hicho.
Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani (kulia) pamoja na Madiwani wa Manispaa ya Bukoba katika kikao hicho.

Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri (kulia) na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh (kushoto) wakiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Bw. Fabian Massawe (kati) katika meza kuu.

Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri (katikati) akimsikiliza kwa makini Bw. Ludovick Utouh.
Viongozi meza kuu wote walikuwa makini  kusikiliza taarifa hiyo ya Ukaguzi.

Taswira ya kikao hicho katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa.Madiwani wa Manispaa ya Bukoba pamoja na Mstahiki Meya Anatory Amani ambaye madiwani wa manispaa wanamtuhumu kwa matumizi mabaya ya madaraka.
(PICHA KWA HISANI YA BUKOBA SPORTS BLOG)

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers