UTATA.......JACK PATRICK KAACHIWA HURU? | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Thursday, January 16, 2014

UTATA.......JACK PATRICK KAACHIWA HURU?Stori: IMELDA MTEMA
UTATA umeibuka kufuatia kuwepo kwa taarifa kuwa huenda modo maarufu aliyedaiwa kushikiliwa nyuma ya ndondo kwa msala wa madawa ya kulevya nchini China, Jacqueline Patrick ameachiwa huru.
Jacqueline Patrick.
Utata huo uliibuka mapema wiki hii mara baada ya akaunti ya modo huyo katika mtandao wa Instagram, kuposti picha mpya za Jack hali iliyowafanya wafusi wa mtandao huo kuamini kwamba yupo huru.
“Haiwezekani mtu awe lupango halafu aweze kuingia Instagram na kuweka picha mpya…au kaachiwa huru?” ilihoji mmoja wa wadau wa mtandao huo.
Baada ya komenti hiyo, wafusi wengi mtandaoni waliweza kuamini kuwa aliyeposti picha hizo ni Jack kwani akaunti iliyotumika ni ileile aliyokuwa akitumia modo huyo.
Mpenzi wa Jack, Jux.
Paparazi wetu naye hakuwa nyuma, alijiridhisha kwa kutazama baadhi ya komenti za kipindi cha nyuma ambazo aliwahi kukomenti katika picha za modo huyo na kuamini kabisa akaunti iliyoposti picha mpya ni Jack.
Wakati tunakwenda mitamboni, mdau mmoja wa burudani alihojiwa na kusema huenda akaunti hiyo ya Jack imetumiwa na msanii wa Bongo Fleva anayefahamika kwa jina la Jux ambaye anatajwa kuwa ni mpenzi wake, alipoulizwa Jux, alisema:
“Jack yupo fresh kabisa niliongea naye…ila amesafiri…”
Jack alidaiwa kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin kilo 1.1 Desemba 19, mwaka jana. Hadi leo sakata lake linawafanya watu wabaki gizani wasijue kinachoendelea.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers