WANAFUNZI BORA WA SAYANSI WAENDA DUBLIN IRELAND | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Wednesday, January 8, 2014

WANAFUNZI BORA WA SAYANSI WAENDA DUBLIN IRELAND


 Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Ireland nchini, Rita Bowen (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi kwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilongelo  ya Singida, Jafari Ndagula mmoja wa washindi wawili wa jumla wa  shindano la Wanasayansi Chipukizi Tanzania 2013 (YST) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Jafari na mwenzake Fidel Samwel (hayupo pichani) wataiwakilisha Tanzania katika sherehe za  Tuzo  za kimataifa za wanasayansi chipukizi duniani mjini Dublin, Ireland. Tuzo za YST  zinadhaminiwa na Ubalozi wa Ireland kwa kushirikiana na Mfuko wa Karimjee Jivanjee Foundation (KJF). Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha na Mwenyekiti wa Mfuko wa KJF, Hatim Karimjee.
 Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Ireland nchini, Rita Bowen (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi kwa mwanafunzi wa Shule ya Fidel Castro ya Zanzibar, Muslih Othman Khamis, mmoja wa washindi wa shindano la Wanasansi Chipukizi Tanzania 2013 (YST) katika hafla iliyonyika jijini Dar es Salaam jana. Tuzo hizo zinadhaminiwa na Ubalozi wa Ireland kwa kushirikiana na Mfuko wa Karimjee Jivanjee Foundation (KJF). Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha na Mwenyekiti wa Mfuko wa KJF, Hatim Karimjee.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers