WATATU WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA GARI......TAHADHARI PICHA ZINATISHA!!! | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Friday, January 31, 2014

WATATU WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA GARI......TAHADHARI PICHA ZINATISHA!!!

Watu watatu akiwemo dereva wa gari ndogo aina ya Ford fiesta nyeusi na wanawake wawili wamepoteza maisha katika ajali mbaya iliyohusisha  gari aina ya Ford fiesta nyeusi na lori aina ya mercedes 1318.

Tukio hili ambalo limetokea katika mji wa Crateus jimbo la kaskazini mashariki nchini Brazili liliripotiwa kuwa ndani ya gari hiyo ya Ford fiesta kulikuwemo na watu watano wanaume watatu na wanawake wawili.
Mmoja ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo
Ubongo wa mmoja wa wahanga wa ajali hiyo ukiwa umetoka nnje

Lori hilo ambalo liligonga  gari dogo kwa upande wa kushoto lilisababisha dereva na wanawake wawili walio kuwa wamekaa siti ya nyuma ya gari hilo kupoteza maisha papo hapo mda mchache baada ya ajali hiyo kutokea.

Katika ajali hiyo vijana wengine wawili kati ya hao watano walijeruhiwa vibaya huku wale waliokuwa katika lori wakitoka salama bila kupatwa na majeraha ya aina yeyote.

Baada ya kutokea kwa ajali  hiyo dereva wa lori hilo aliwaita watu wa huduma ya kwanza katika eneo la tukio kwaajili ya kutoka msaada.

Polisi walipo fika katika eneo la tukio waliwachukua majeruhi pamoja na dereva wa lori hilo kwaajili uchunguzi zaidi. 
gari ndogo aina ya Ford fiesta nyeusi likiwa limeharibika vibaya baada ya kugongwa na lori hilo
Dereva wa gari ndogo  aliye poteza maisha
Lori lililo sababisha ajali hiyo likiwa limepinduka

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers