WAZIRI MKUU PINDA ATUA DARAJA LA DUMILA | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Thursday, January 23, 2014

WAZIRI MKUU PINDA ATUA DARAJA LA DUMILA


Daraja la Dumila wilayani Mvomero, Morogoro likiwa limekatika baada ya kunyesha mvua kubwa.
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda hivi punde amewasili eneo la daraja la Dumila mkoani Morogoro lililokatika baada ya kunyesha mvua kubwa ili kujionea hali halisi ya eneo hilo pamoja na kutoa pole kwa familia zilizokumbwa na maafa hayo.
Mhe. Pinda ametua kwa helkopta ya polisi na ameungana na Waziri wa Ujenzi, Mhe. John Pombe Magufuli aliyetangulia eneo hilo.
Mpaka sasa hakuna magari yanayopita eneo hilo kutokana na kukatika kwa daraja hilo ambalo ni kiunganishi kati ya mkoa wa Dodoma na Morogoro.
(Habari: Dustan Shekidele / GPL, DUMILA)

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers