Yanga yabariki kuondoka kwa Niyonzima | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Wednesday, January 22, 2014

Yanga yabariki kuondoka kwa Niyonzima
Haruna Niyonzima.
Na Khadija Mngwai
UONGOZI wa Klabu ya Yanga umefunguka kuwa, hauna kipingamizi cha aina yoyote juu ya kiungo mshambuliaji wake, Haruna Niyonzima, aliyetangaza kuondoka iwapo dili lake litakamilika.
Niyozima aliliambia Championi hivi karibuni kuwa yupo katika mchakato wa kuiacha timu hiyo iwapo mikakati yake itakamilika kwa kuwa kuna klabu kadhaa zinamfuatilia.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb, alisema uongozi upo tayari kumtoa mchezaji yeyote yule iwapo taratibu zitafuatwa na hawatakuwa na kipingamizi iwapo Niyonzima, raia wa Rwanda, atatakiwa.

“Iwapo timu yoyote itakuwa tayari kumsajili Niyonzima tutakuwa tayari kumruhusu ilimradi tu wafuate utaratibu unaotakiwa na si vinginevyo.
“Na si Niyonzima tu, bali hata mchezaji mwingine yeyote yule akijiona anataka kuondoka tutamruhusu kwani lengo letu ni kuona wachezaji wanafanikiwa kusonga mbele zaidi kisoka,” alisema Bin Kleb.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers