ANGALIA PICHA MTOTO WA MAAJABU ALIYEZALIWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA SINGIDA.

Mtoto mchanga aliyezaliwa  akiwa hana mikono, kifua, shingo na kichwa, ila ana anasehemu ya miguu , makalio na tumbo akiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida muda mfupi baada ya kuzaliwa na Bi. Amina Bilau mkazi wa  kijiji cha Mtamaa tarafa ya Mwakonko manispaa ya Singida
. (Picha na Nathaniel Limu). 
Na Nathaniel Limu.
Mtoto mchanga amezaliwa katika  hospitali ya mkoa wa Singida akiwa hana baadhi ya sehemu za mwili kuanzia kifuani hadi kichwani.
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Dkt. Joseph Malunda, amesema hospitali ya mkoa wa Singida ni mara ya kwanza kuzaliwa kiumbe kama hicho tangu kuwa hospital ya mkoa.
Dkt. Malunda amesema watoto hao ambao wamezaliwa mapacha wote wa kike wakiwa na miezi saba,  mmoja ambaye ana viungo vyote  alikuwa na kilo 1.3  lakini alifariki  baada ya saa sita kupita.
Dkt. Malunda amesema baada ya mama mzazi wa watoto hao Amina Bilau kujifungua mtoto wa kwanza, waliona mtoto mwingine akifuatia na ndipo alipojifungua kitoto hicho chenye kilo 1.4  ambacho hakina mikono ,kifua,na kichwa  
Kutokana na hali hiyo  Dkt. Malunda amewashauri wakina mama wanapopata uja uzito kuhudhuria kliniki na kuacha kutumia madawa makali pindi wanapokuwa wajawazito.
Dk. Malunda amesema madawa ya aina hiyo yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuzaliwa watoto ambao wanakuwa na mapungufu ya viungo.
Akieleza huku akiwa amelazwa katika hospita ya mkoa wa Singida mama huyo Amina  Bilau  ambaye  ni mkazi wa  kijiji cha Mtamaa kata ya Mwankoko  Manispaa ya Singida,  amesema yeye  aliona tumbo lina kuwa kubwa na baada ya kupata matibabu katika zahanati ya kijiji  bila mafanikio aliamua kwenda katika hospita ya mkoa wa Singida na kijifungua watoto akiwa katika hali hiyo.

Kwaupande wake baba wa watoto hao  Maulidi Mkuki alipohojiwa, amesema anashangaa  kuona mke wake amejifungua mtoto wa aina hiyo  wakati yeye ana watoto wengine watatu ambao  wamezaliwa bila ya kuwa na matatizo yo yote.
Katika hatua nyingine wagonjwa walio fika kutibiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida mchungaji  wa kanisa la Anglikana Harodi Ibuku na mkazi wa Singida  Atanas Malya, wamesifu madakta kuendele kutoa huduma.
 Wamewashauri  kumsikiliza Rais Jakaya Kikwete  baada ya kuhutubia Taifa na  kuwataka kusitisha mgomo na kuendelea kutoa huduma ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
ANGALIA PICHA MTOTO WA MAAJABU ALIYEZALIWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA SINGIDA. ANGALIA PICHA MTOTO WA MAAJABU ALIYEZALIWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA SINGIDA. Reviewed by Linnah Lsquare on 1:32 AM Rating: 5
Powered by Blogger.