HTARI SANA.....UKIKUTANA NA MTU HUYU, KAA MBALI! | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Friday, February 28, 2014

HTARI SANA.....UKIKUTANA NA MTU HUYU, KAA MBALI!

Stori: MWANDISHI WETU
Kuna mtu mmoja almaarufu kwa jina la Kamanda au Kachero wa OFM (Oparesheni Fichua Maovu) ya Global Publishers ambaye unashauriwa ukikutana naye kaa mbali, pata undani wake.

Kamanda au Kachero wa OFM (Oparesheni Fichua Maovu).
Jamaa huyo hatari amedhamiria kuibadili Tanzania kimaadili kwa kuibua na kufichua uovu katika jamii.
Tayari amefanya matukio mengi makubwa ya kufichua uovu ndani na nje ya Jiji la Dar.
KIVIPI?
Anachokifanya Kamanda wa OFM ni kwamba hupokea ujumbe wenye harufu ya uovu au kero katika eneo la mtumaji kwenye magazeti ya Global Publishers kisha huifanyia kazi.
Baada ya kupokea ujumbe wa aina hiyo kwenye namba zilizopo kwenye magazeti hufanya uchunguzi wa kina usiku na mchana.
Kamanda wa OFM akishajiridhisha kuwa uovu huo unatendeka hujipanga kwa kuandaa mwongozo (script) ili kufanya oparesheni na kuuanika uovu huo.
USHUHUDA WA BABA JOY
“Ukweli ni kwamba jamaa huwa hakurupuki na huwa hakosei. Usiombe ukutane naye au akufuatilie. Jamaa ni mtu hatari lakini alinisaidia sana.
“Ndoa yangu ilikuwa ivunjike lakini alimfuatilia mke wangu hadi nikapata ushahidi kwani mama watoto alikuwa akikataa katakata kuwa hanisaliti.
“Kweli baada ya kupata ushahidi mke wangu alikiri na kuomba msamaha na sasa maisha yanaendelea. Mimi namvulia kofia Kamanda wa OFM,” alisema Baba Joy, mkazi wa Sinza, Dar.
Mke wa Baba Joy (Mama Joy) aliwahi kunaswa na Kamanda wa OFM kwenye jaribio la kusaliti ndoa na mwanaume mwingine kwenye gari.

MATUKIO YA KUKUMBUKWA YA KAMANDA WA OFM
Yapo matukio mengi yaliyotekelezwa na Kamanda wa OFM na hapa tunakukumbusha machache;
DOKTA MAMBO
Mapema mwaka huu Kamanda wa OFM alifanikisha tukio la kunaswa kwa daktari aliyejulikana kwa jina moja la Mambo maarufu sana kwa jina la Dokta Mambo ambaye alikutwa katika jaribio lililodaiwa kuwa ni la utoaji mimba.
Wakati Kamanda wa OFM akichora ramani ya namna ya kumnasa dokta huyo kwenye zahanati yake iliyopo Kawe jijini Dar, watu wengi hasa wanawake walidai jamaa huyo hanasiki lakini alinaswa hivyo kutibu ‘ugonjwa’ wa utoaji mimba.
BABU NA DENTI
Wiki kadhaa zilizopita, Kamanda wa OFM alimnasa babu aliyetajwa kwa jina moja la mzee Omari, akiwa gesti na denti wa shule moja ya sekondari jijini Dar (jina la denti na shule vinahifadhiwa kimaadili).
Tukio hilo la aibu lilijiri kwenye gesti moja iliyopo maeneo ya Kawe, Dar na kusababisha timbwili zito hivyo kuibua na kukemea ile tabia ya ‘vibabu’ kupenda kutembea na dogodogo.
MFANYABIASHARA WA MAGARI
Tukio lingine la kuibua maovu, hivi karibuni Kamada wa OFM alifanikiwa kumnasa mfanyabiashara maarufu wa magari jijini Dar, aliyefahamika kwa jina moja la Juvenali akiwa katika jaribio la ulawiti kwa
‘modo’ maarufu Bongo (jina tunalihifadhi).
KAUMBA, MOROGORO
Kwa kushirikiana na polisi, hivi karibuni Kamanda wa OFM alitinga mkoani Morogoro ambapo alifanikisha kufumuliwa kwa eneo korofi kwa biashara haramu ya ngono la Kaumba na kwenye malori pale Msamvu.
MKE WA RAFIKI
Ukiangalia ukurasa wa nyuma wa gazeti hili, Kamanda wa OFM amefanikisha kunaswa kwa mwanamke mmoja aliyekuwa kwenye jaribio la kusaliti kwa rafiki wa mumewe ambaye pia ni rafiki wa mume wa aliyenaswa.
KAZI NDIYO IMEANZA
Akizungumzia kazi yake hiyo ya kufichua maovu, Kamanda wa OFM alikuwa na haya ya kusema: “Ndiyo kwanza kazi imeanza.
“Kwa yeyote mwenye taarifa ya uovu au ufisadi unaofanyika awasiliane na mabosi zangu kupitia namba zao kwenye magazeti.
“Nikishainyaka hiyo taarifa, nawaahidi kuwa sikosei, nitawafanyia Watanzania kazi nzuri. Nimepania kuibadili Tanzania kwa kuwa uovu unazidi kuongezeka kila kukicha.” 

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers