LULU AKUMBUKA MAPENZI YA KANUMBA VALENTINE’S DAY!! | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Sunday, February 16, 2014

LULU AKUMBUKA MAPENZI YA KANUMBA VALENTINE’S DAY!!

Stori:  Mayasa Mariwata
WAKATI kesi yake juu ya kifo cha aliyekuwa nyota wa filamu Bongo, Steven Kanumba ikianza kurindima leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa la moyoni akikumbuka mapenzi ya jamaa huyo aliyetangulia mbele za haki.

Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Lulu alifunguka hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) iliyosherehekewa duniani kote Ijumaa iliyopita.

Marehemu Steven Kanumba.
“Kuna mtu natamani kumtakia Happy Valentine’s Day kwa kuwa nakumbuka mapenzi yake kwangu lakini kwa bahati mbaya siwezi kwa sababu hayupo na haiwezekani tena,” alisema Lulu.
Hata hivyo, alipobanwa amtaje, staa huyo ambaye ni sura ya mauzo ya filamu za Kibongo alikiri kuwa ni Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, 2012, siku ambayo kamwe hawezi kuisahau maishani mwake.
 credit:GPL

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers