MAMA KANUMBA AMBARIKI WEMA

Hamida Hassan na Gladness Mallya
SIKU chache baada ya mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa kukiri kwamba Elizabeth Michael ‘Lulu’ alikuwa mkwe sahihi kwake, safari hii ameibuka na kumbariki Wema Sepetu ambaye naye aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaye, akisema ana huruma, roho nzuri na utu.
 
Mama Kanumba, Flora Mtegoa.
Akizungumza kwa kujiamini, mama Kanumba alisema: “Hili nalizungumza kutoka moyoni mwangu, huyu mtoto ana moyo wa upendo sana. Angalia namna anavyowasaidia wenzake wanapopata matatizo. Anajitoa kwa moyo, siyo mchoyo. Kwa kweli Mungu amwongezee.”Wema Sepetu.
“Kiukweli Wema anajitoa sana... nakumbuka hata kipindi akiwa na mwanangu, maana uhusiano wao niliutambua, Kanumba mwenyewe alinitambulisha; walikuwa wakija kunisalimia nyumbani ananiita pembeni na kunipa pesa ili Kanumba asione, akitaka na yeye anipe. Huo ni moyo wa kipekee sana,” alisema mama huyo.
Hiki ni kama kipindi cha mama huyo kuonesha hisia zake kwa wakwe zake (wasichana waliowahi kuwa na uhusiano na marehemu mwanaye) kwani takribani wiki tatu zilizopita, alimzungumzia Lulu kwa maelezo kuwa alikuwa mkwe sahihi kwake.

Credit:GPL
MAMA KANUMBA AMBARIKI WEMA MAMA KANUMBA AMBARIKI WEMA Reviewed by Linnah Lsquare on 2:01 AM Rating: 5
Powered by Blogger.