MASKINI...MIMBA YA MSANII LINAH YACHOROPOKA...SOMA ZAIDI HAPA... | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Thursday, February 27, 2014

MASKINI...MIMBA YA MSANII LINAH YACHOROPOKA...SOMA ZAIDI HAPA...

SIKU chache baada ya kuripotiwa kuwa, msanii wa Bongo Fleva, Astelinah Sanga ‘Linah’ amenasa ujauzito wa mdosi aitwaye Nagar, Amani limenyetishiwa kuwa ujauzito huo umechoropoka. 

Astelinah Sanga ‘Linah’.
 Kwa mujibu wa chanzo, ujauzito huo umechoropoka hivi karibuni na kumfanya  Linah 
kukosa raha kwa kuwa ndoto yake ilikuwa kupata mtoto.

 “Ni kweli Linah alikuwa na ujauzito lakini umetoka na amesikitika sana kwani mdosi wake
 ni mtu mwenye fedha nyingi na yeye alitamani sana kuwa na mtoto,” kilisema chanzo hicho. 

Gazeti hili lilimtafuta Linah  kupitia simu yake ya kiganjani ili kupata ukweli wa kutoka kwa ujauzito huo lakini baada ya mwandishi wetu kujitambulisha, staa huyo alikata simu. 

Wiki iliyopita gazeti dada na hili, Risasi Mchanganyiko la Februari 19-21, mwaka huu 
liliandika habari za staa huyo kunasa  ujauzito  wa mdosi huyo na alipoulizwa alisema habari hizo zilikuwa ni uzushi. 
“Nani kakwambia kwamba nina  mimba? Hayo ni maneno ya watu, wanasambaza mitaani 
sijui hata wameyatoa wapi lakini miye sina mimba,” alisema Linah na kunukuliwa na gazeti 
hilo ambalo hutoka mtaani kila siku ya Jumatano likiwa na habari motomoto za masupastaa.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers