MATAJIRI WANUNUA MABAO YANGA!!! | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Tuesday, February 25, 2014

MATAJIRI WANUNUA MABAO YANGA!!!

Lucy Mgina na Martha Mboma
WANACHAMA wa Yanga Family wameahidi kununua kila bao litakalofungwa kwenye mechi ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly itakayopigwa Jumamosi ya wiki hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Yanga ilifanikiwa kuingia raundi ya kwanza ya michuano hiyo baada ya kuitoa Komorozine ya Comoro kwa jumla ya mabao 12-2.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo kilisema kuwa kundi la Yanga Family limejipanga kuhakikisha linanunua mabao watakayofunga katika mchezo huo ili kuongeza ari kwa wachezaji watakapokuwa wakipigana uwanjani.
Ripoti hizo zinasema zaidi kwamba licha ya kutambua mechi hiyo itakuwa ngumu kwa upande wao, wameamua kutumia njia hiyo kama sehemu ya kuwashawishi wachezaji wacheze kwa nguvu na morali kubwa ili wavunje rekodi ya kuwaondoa Waarabu hao mapema kwenye michuano hiyo mikubwa Afrika kwa ngazi ya klabu.
Mbali na ahadi kutoka kwa wanachama hao, uongozi umejipanga kuhakikisha unawapa zawadi kubwa iwapo wataibuka na ushindi kwenye ardhi ya Tanzania.
 “Suala la ahadi hakuna tatizo kwa kuwa kamati husika zimejipanga na kila kitu kipo sawa, vikao vya kuijadili mechi hiyo vinaendelea kila siku, lengo ni kutaka kufanya vizuri.
“Tayari Yanga Family wameahidi kununua kila bao watakalofunga,  lakini uongozi wa juu haujataka kusema utakachotoa kwa kuwa wanaona kama watawaharibu kisaikolojia wachezaji japokuwa zawadi ipo tena  kubwa tu!,” kilisema chanzo hicho.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers