MICHELLE OBAMA AFUNGUKA KUHUSU TABIA CHAFU ZA JUSTINE BIEBER...SOMA ZAIDI HAPA...! | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Wednesday, February 12, 2014

MICHELLE OBAMA AFUNGUKA KUHUSU TABIA CHAFU ZA JUSTINE BIEBER...SOMA ZAIDI HAPA...!

Justin Bieber ni msanii ambaye amekuwa katika vichwa vingi vya habari miezi kadhaa ya karibuni, sio kwasababu ya kazi nzuri anayoifanya bali ni kutokana na vurugu na uvunjaji wa sheria wa kupita kiasi, kiasi kwamba hivi karibuni wananchi wa Marekani wamempigia kura (Deport Bieber Petition) ya kuiomba serikali imrudishe kwao sababu wamechoshwa na tabia zake.

Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama ametoa ushauri kwa wazazi wa msanii huyo, akijitolea mfano kama yeye ndio angekuwa mzazi wa Bieber (19), kwa kueleza kile ambacho angejaribu kufanya kumsaidia mwanaye katika kipindi hiki ambacho ameonekana kuwa na changamoto nyingi zinazoonekana kusababishwa na umri wake (foolish age). 

First Lady amesema kama yeye angekuwa mzazi wa Bieber angejaribu kuwa naye karibu muda wote, na kuzungumza naye na kumshauri.

“Mimi ningekuwa karibu naye sana kwenye maisha yake katika kipindi hiki….kuongea naye, ili kujua nini kinaendelea katika kichwa chake, na kujua nani yuko katika maisha yake na nani hayuko.” Alisema Michelle katika mahojiano ya hivi karibuni na kituo cha Univision Radio.

Kuna uwezekano ushauri wa first lady ni siri ya mafanikio ya malezi bora wanayoyapata mabinti zake wawili Sasha na Malia, ambao pamoja kuwa ni watoto wa Rais wa taifa kubwa duniani lakini wanaonekana kuwa na nidhamu.
”[Kids] just want you near, you know — they want that advice from a parent. They want to see you on a daily basis, because the thing is he’s still a kid. He’s still growing up. So, I would pull him close.” Aliongeza Michelle.
credit:Kandili yetu

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers