Ni pale mwanaume anapoonyesha tamaa kubwa ya ngono na kulazimisha kukutana kimwili wakati mwanamke aliweka msimamo wa kutokutana kimwili na mwanaume yeyote mpaka baada ya muda fulani tangu kufahamiana na kuwa wachumba au mpaka pale watakapofunga ndoa.Huu ni mtihani kwa wanawake wengi kwa sababu unawaweka katika wakati mgumu wa kuchagua kuvunja nadhiri waliojiwekea au kusimama imara kwenye msimamo waliyojiwekea kwa ajili yakulinda heshima zao.

Swali kwa wanawake: Je unapokabiliwa na mtihani kama huu ni uamuzi gani unaona ni sahihi kwako….?