PICHA ZINATISHA...UKATILI MKUBWA DAR...KIBAKA APOKEA KICHAPO KIKALI TOKA KWA WANANCHI WENYE HASIRA KALI...!! | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Thursday, February 27, 2014

PICHA ZINATISHA...UKATILI MKUBWA DAR...KIBAKA APOKEA KICHAPO KIKALI TOKA KWA WANANCHI WENYE HASIRA KALI...!!

Kutokana na hasira za watu hao walioamua kujichukulia sheria mkononi,sidhani kama alipona kwani baadaye walitokea mgambo wa jiji na kumuokoa, Wakati wakielekea katika kituo cha Polisi cha Karume Kibaka huyo alianguka na kupoteza fahamu kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi kichwani.


Mmoja wa wananchi mwenye hasira kali akimponda na tofari Kibaka ambaye jina lake halikujulikana mara moja baada ya kudaiwa kumkwapua abiria mmoja aliyekuwa ndani ya gari akisafiri kuelekea Mwenge akiwa ametokea Tandika.
Kibaka huyo inadaiwa alimkwapua simu abiria huyo na kukimbilia katika eneo la makaburi yaliyopo Karume na ndipo lilipoibuka kundi la Watu na kuanza kumfukuza na hatimaye kufanikiwa kumkamata na kuanza kumshushia kibano cha nguvu kama uonavyo pichani.  
Blog hii inalaani na itazidi kulaani matukio kama haya,ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi na kupoteza uhai wa wenzao kirahisi hivi,ilhali sheria zipo.Mungu Ibariki Afrika,Mungu Ibariki Tanzania.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers