STAA WA FAST & FURIOUS, PAUL WALKER AACHA URITHI WA DOLA MILIONI 25 KWA BINTI YAKE…


Staa wa filamu za Fast & Furious, Paul Walker alifariki kwa ajali mbaya ya gari mwezi Novemba mwaka jana. Mara tu baada ya kifo chake, watu wengi walikuwa na maswali je utajiri wake aliokuwa nao atauacha kwa nani? Sasa imefahamika kuwa ameacha urithi wenye thamani ya Dola za kimarekani Milioni 25
WALKER2
Familia ya Fast & Furious…
Kupitia mtandao wa TMZ, umesema Wosia aliouandika Paul Walker kabla ya mauti kumfika, umeeleza kwamba mali zote ambazo mkali huyu alikuwa nazo zitabaki kwa binti yake wa miaka 15, aitwaye Meadow.
MEADOW

Paul Walker akiwa na mwanae, Meadow…
Matarajio ya wengi yalikuwa, kungekuwa na mgao mzuri ambao kwa upande mmoja ama mwingine ungemnufaisha mpenzi wake Walker aliyedumu naye kwa muda wa miaka saba,Jasmine Gosnell lakini mambo hayakwenda kama walivyodhani.
Kwa sasa, Meadow anaishi Hawaii na mama yake, Rebecca Soteros japo wosia ulimtaka aishi na mama yake Paul Walker,Cheryl kwani ndiye mwenye haki ya malezi na matunzo yote.
credit :GongaMx
STAA WA FAST & FURIOUS, PAUL WALKER AACHA URITHI WA DOLA MILIONI 25 KWA BINTI YAKE… STAA WA FAST & FURIOUS, PAUL WALKER AACHA URITHI WA DOLA MILIONI 25 KWA BINTI YAKE… Reviewed by Linnah Lsquare on 4:48 AM Rating: 5
Powered by Blogger.