TABIA ZA WANAUME ZISIZOWAPENDEZA WANAWAKE!!!!SOMA HAPA UKAJIREKEBISHE!! | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Tuesday, February 4, 2014

TABIA ZA WANAUME ZISIZOWAPENDEZA WANAWAKE!!!!SOMA HAPA UKAJIREKEBISHE!!


1. Aina ya kwanza ni ile ya mwanaume ambaye anatatabirika. Wanawake hawapendi wanaume wanaotabirika kwa sababu wanaelewa ni jinsi gani watalipokea jambo lolote linalotokea. Mwanamke anaweza kujua kabisa kwamba, leo atatolewa outing au hapana, ataletewa zawadi au la. Yaani hakuna kitu tunachokiita surprise. Wanawake wanataka kiasi fulani cha kutotabirika toka kwa wanaume. Ndio maana utakuta anaishi au kuolewa na mwanaume jeuri au mwenye roho mbaya . siyo kwamba anampenda kwa jeuri yake, bali kwa kutotabirika kwake.
2. Aina ya pili ni ile ya mwanaume anayejisikia (mwenye maringo). Huyu kwa kawaida ni mbinafsi sana. Ni jeuri siyo kwa mpenzi wake tu, bali hata kwa mtu yeyote ambaye anamuona yuko chini yake. Kuwaringia watu wengine ni sawa na kumringia mpenzi wako moja kwa moja.
3. Aina ya tatu ni ile ya wanaume jeuri. Mtu jeuri hana aibu! Wakati mwingine anaonesha waziwazi kwamba anamtamani mwanamke mwingine mbele ya mpenzi wake! Anafikia hatua ya kumsimulia mpenzi wake kuhusu marafiki zake wa kike wa zamani na hata u.p.u.u.z.i waliokuwa wakifanya! Kwa ujumla anawadharau wanawake.
4. Aina ya nne ni ile ya mwanaume bahili. Hamnunulii mpenzi wake zawadi hata siku moja! Kila wakati watokapo outing yeye na mpenzi wake huagiza vyakula vya bei rahisi sana pamoja na kwamba, anazo hela. Anataka kumfanya huyo mpenzi wake atishike naye aagize vya bei rahisi. Na wakati wa kulipa anahesabia fedha mfukoni, anatoa fedha utadhani bajeti inabana sana au utadhani yeye na mpenzi wake wamekubaliana “kukaza mikanda.” Mwanaume anaonesha ana mkono wa birika namna hiyo katika siku za kwanza tu za mapenzi! Je huko baadaye itakuwaje? Si atahesabu hata vipande vya nyama jikoni!
5. Aina ya tano ni ile ya mwanaume mbishi. Hata majadiliano ya kawaida tu, yeye anataka kubishana! Anapomtoa outing mwanamke, anakuwa kama amempeleka kwenye mashindano ya mdahalo! Mwanamke hajisikii kuwa huru kutoa maoni au kusema hisia zake, maana atabishiwa.
6. Aina ya sita ni ya mwanaume asiyekosea. Huyu bwana anapenda sana kuhumu wenzie. Inawezekana hanywi wala havuti sigara, anataka hata wenzie wamuige yeye, wasinywe wala wasivute sigara. Toka siku ya kwanza anayotoka na mwanamke anaanza kumhubiria anayoyataka yeye, siyo asiyoyataka mwanamke. Huyu hataki kabisa mwanamke akawa huru kama yeye, bali angependa yeye amuamulie awe nani na afanye kipi au asifanye kitu gani, ebo! Sasa hapo ni mtu na mpenzi wake au mtu na mtumwa wake!
7. Aina ya saba ni ile ya mwanaume kuwachukia wanawake. Hafichi chuki yake kwa wanawake. Huyu huonesha dhihaka nyingi kwa mpenzi wake na kuwaponda wanawake kwa ujumla wao. Mazungumzo yake yote yatakuwa ni kuwadharau, kuwadhalilisha na kuwanyanyapaa wanawake. Hivi ni mwanamke wa namna gani ambaye atamkubalia mwanaume mpondaji namna hii? Labda mwanamke mwenye mkabala wa kufujwa peke yake au yule mwenye kutaka tu kuchuna buzi na kusepa zake.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers