WEMA AWASHANGAA WANAOMPONDA JOKATE BAADA YA KUMALIZA TOFAUTI ZAO, SOMA ALICHOKISEMA HAPA!!!

Mwigizaji Wema Sepetu, amewashangaa wanaomponda Jokate Mwegelo kwa kumaliza tofauti baina yao akisema kuwa hawatendi haki na wanaingilia uhuru wa wasanii hao.
Kauli ya Wema imekuja siku chache baada ya Jokate kufika kwa kushtukiza katika onyesho lililofanywa na Wema mkoani Arusha hivi karibuni na kumaliza tofauti zao.
Wawili hao wanadaiwa walikuwa wakimgombea mwanamuziki nyota na tajiri, Diamond Platinum.
“Sikuona kioja wala ajabu, kwa kuwa tulikuwa marafiki na kilichotokea ni ujana. Kila mmoja amekaa na kuona hakuna haja ya kuwa na bifu zisizokuwa na faida. Nimemuunga mkono Jokate kwa kuwa ameonyesha kukua na kukomaa kiuamuzi, hakuna haja ya kumbeza kwa maneno ya kijinga,”alisema Wema.

credit:Bongoclantz 
WEMA AWASHANGAA WANAOMPONDA JOKATE BAADA YA KUMALIZA TOFAUTI ZAO, SOMA ALICHOKISEMA HAPA!!! WEMA AWASHANGAA WANAOMPONDA JOKATE BAADA YA KUMALIZA TOFAUTI ZAO, SOMA ALICHOKISEMA HAPA!!! Reviewed by Linnah Lsquare on 10:04 PM Rating: 5
Powered by Blogger.