ZIJUE SABABU ZA WANAWAKE WANAOSHINDWA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA!!!!


Kuna matatizo mengi yanayohusiana na tendo la kujamiiana, ambayo yanawakabili wanawake. Matatizo haya ni yale ambayo yanamzuia mwanamke kushiriki kwenye tendo la kujamiiana na kupata ridhiko au kumfanya kutoweza kushiriki kwa muda fulani au kwa kudumu.

Ukilinganisha, wanawake wana matatizo makubwa zaidi yanayohusiana na tendo la kujamiiana, kuliko wanaume. Wanawake hukabiliwa na matatizo haya kwa asilimia 45 wakati wanaume hukabiliwa kwa silimia 30. Bahati mbaya hata hivyo ni kwamba, matatizo yote yanayohusiana na tendo la kujamiiana huwa hayajadiliwi na wapenzi waziwazi au pengine hayajadiliwi kabisa. Kama yakijadiliwa mara nyingi inakuwa ni kwenye sura ya lawama, kashfa, na mengine ya aina hiyo, ambayo husaidia kuvuruga uhusiano. Matatizo yanayohusiana na tendo la kujamiiana husababishwa na mambo mbalimbali, lakini naweza kuyagawa katika makundi makubwa mawili. Kundi la kimwili na kundi la kisaikolojia.

Kwa mfano mtu mwenye kisukari anaweza kukabiliwa na ugumu kwenye tendo la ndoa, mwenye maradhi ya moyo pia, mwenye hitilafu ya uwiano wa homoni mwilini, anaweza kukabiliwa na matatizo haya. Mengine ni pamoja na maradhi sugu ya figo na ini, yaani viungo hivyo kushindwa kufanya kazi zake vizuri, unywaji mkubwa wa pombe au matumizi ya madawa ya kulevywa au vidonge vya kawaida, vikiwemo vile vinavyoitwa vya majira na vile vya kukabiliana na sononi. Matatizo ya kisaikolojia ni pamoja na sononi za kikazi au kimaisha, hofu kuhusu tendo la kujamiiana, matatizo ya ndoa au uhusiano, yaani migogoro katika ndoa au uhusiano, kushtakiwa na dhamira, kumbukumbu mbaya za nyuma kuhusiana na tendo la kujamiiana.


Wanawake kama nilivyosema, ndio ambao hukabiliwa zaidi na matatizo yanayohusiana tendo la kujamiiana. Moja ya matatizo haya ni ile hali ya kukosa hamu ya tendo ambayo inadaiwa kwamba inawakabili wanawake wengi sana kuliko inavyofikiriwa. Miongoni mwa sababu za tatizo hili ni mabadiliko ya kihomoni, matumizi ya dawa za aina fulani, sononi za kimaisha au kindoa, ujauzito, uchovu na sababu nyingine zinazofanana na hizo. Hata ile hali ya kuwa na mtindo mmoja na aina moja ya kufanya mapenzi, huweza kumwondolea mwanamke hamu ya tendo. Kuna wakati wanawake hawana hamu kwa sababu wanaume wanaoshiriki nao wameshindwa kuwafanya wakafika mahali ambapo watakuwa na hamu. Kuna wanaume ambao hawajui kuwaandaa wapenzi wao, hivyo kuwafanya kukosa hamu kabisa na tendo hilo.

Tatizo lingine ni lile la mwanamke kushindwa kufika kileleni. Hili huweza kusababishwa na mwanamke kukosa uzoefu, hofu, kushtakiwa na dhamira, kumbukumbu isiyopendeza ya kilichotokea nyuma kuhusiana na tendo la kuamiiana, matumizi ya dawa au maradhi sugu ambayo mwanamke anayafahamu au hajui kwamba anayo. Halafu kuna tatizo la maumivu, ambapo mwanamke huhisi mauamivu wakati akishiriki tendo. Hapa kuna sababu nyingi, ni kwa nini mwanamke anaweza kuhisi maumivu wakati wa tendo. Mengi ni yale yanayohusiana na hitilafu kwenye maumbile ya mwanamke, yaani sehemu zake za siri au maeneo yaliyo karibu. Lakini hata maradhi ya zinaa yanaweza kufanya mwanamke kuhisi maumivu wakati wa kujamiiana.Wakati mwingine kovu la mshono sehemu za siri au karibu na hapo huweza kusababisha kitendo cha kujamiiana kuwa na maumivu kwa mwanamke. Kuna hali ambayo kitaalamu hufahamika kama vaginismus, ambapo msuli wa maeneo ya sehemu za siri husinyaa wakati mwanamke anapokaribia kufanya tendo. Hali hii mara nyingi huwapata wanawake ambao wanahofia kwamba kuingiliwa kutawapa maumivu. Inaweza ikawa pia ni sababu ya hofu ya ziada ya tendo ambayo haina sababu ya msingi. Wakati mwingine inaweza kuwa ni sababu ya kumbukumbu mbaya kuhusu tendo la kujamiiana ambayo ilimtokea mhusika.

Tiba ya matatizo haya ipo, lakini ni lazima kwanza ifahamike yanasababishwa na kitu gani ili iwe rahisi kupendekezewa tiba, kwani kuna tiba za hospitali ambazo ni za kutibu mwili na kuna zile za ushauri wa kisaikolojia. Kuna wakati zote ni muhimu kwenda pamoja.

ZIJUE SABABU ZA WANAWAKE WANAOSHINDWA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA!!!! ZIJUE SABABU ZA WANAWAKE WANAOSHINDWA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA!!!! Reviewed by Linnah Lsquare on 2:02 AM Rating: 5
Powered by Blogger.