BREAKING NEWZZ..BOTI YAZAMA NA KUUA WATU 25 AMBAO NI WAKIMBIZI...SOMA ZAIDI HAPA... | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Sunday, March 23, 2014

BREAKING NEWZZ..BOTI YAZAMA NA KUUA WATU 25 AMBAO NI WAKIMBIZI...SOMA ZAIDI HAPA...

MIILI 25 imepatikana Ziwa Albert baada ya boti iliyokuwa imebeba wakimbizi wa Jamhuri
 ya Kidemokrasia ya Kongo kuzama. Wakimbizi hao walikuwa wakitoroka kutoka kambi ya wakimbizi ya Kyangwali wilayani Hoima magharibi mwa Uganda, wakirejea kwao.

 Kwa sasa Jeshi la polisi linaendelea na jitihada za kutafuta miili zaidi. Kamanda wa polisi 
wa eneo hilo John Ojukuna amesema watu 43 wameokolewa. Boti iliyozama inadhaniwa 
kuwa ilikuwa imebeba zaidi ya wakimbizi 100.

 Wengi wa wakimbizi hao ni wale waliokimbia mapigano mashariki mwa Kongo mwaka jana. 

Mwendeshaji wa boti hiyo amekamatwa na jeshi la polisi na inadaiwa kuwa alikuwa 
amelewa. Wakimbizi waliookolewa wamewaambia polisi kuwa alikuwa mlevi na alikuwa akiendesha boti hiyo kwa kasi. 
Hii siyo mara ya kwanza ajali ya boti kuua watu katika Ziwa Albert kutokana na kujaza
 abiria na mizigo kupita kiasi. Miaka minne iliyopia boti nyingine ilizama na kusababisha vifo vya watu
-via kandili yetu

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers