HAYA SASA NI MAKUBWA NA MAZITO........DOGO JANJA NA ASLAY WAVUNJA UCHUMBA WA WATU MKOANI MTWARA...SOMA ZAIDI HAPA... | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Wednesday, March 12, 2014

HAYA SASA NI MAKUBWA NA MAZITO........DOGO JANJA NA ASLAY WAVUNJA UCHUMBA WA WATU MKOANI MTWARA...SOMA ZAIDI HAPA...

MADOGO wanaotikisa katika ulimwengu wa muziki Bongo, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ na Asilahi Isihaka ‘Aslay’ wamedaiwa kuvunja uchumba wa jamaa aliyefahamika kwa jina la Fikiri Chodas na Farida.

Asilahi Isihaka ‘Aslay’.
 Tukio hilo lilitokea usiku wa Machi 7, mwaka huu, Newala mkoani Mtwara wakati wasanii hao walipokuwa wamekwenda kufanya ziara ya kimuziki.

 Kwa mujibu wa chanzo makini, baada ya madogo hao kufanya shoo kali mjini humo, Farida aliwang’ang’ania wasanii hao waliokuwa wakijiandaa kwenda kulala katika hoteli waliyofikia ndipo Fikiri alipokasirika.
 Uvumilivu ulimshinda Fikiri, akamvaa Dogo Janja na kumtaka aachane na mpenzi wake, mchumba wake huyo naye akaja juu na kuhamia kwa Aslay ndipo vurugu ilipotokea ambapo Fikiri alihangaika kumkwida ili kumuokoa mpenzi wake asiondoke na wasanii hao.
 

Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’.
 Kuonesha mwanamke huyo alikuwa ‘amekolea’ kwa wasanii hao, alianza kumporomoshea mpenzi wake matusi ya nguoni na kudai amuache kwani ‘wametembea’ naye siku moja tu.
 Fikiri alipoona mpenzi wake huyo anamkana, aliamua kutangaza kummwaga papo hapo.
Jitihada za mapaparazi wetu kufuatilia sakata hilo kwa undani zilizaa matunda baada ya kufanikiwa kunasa video ya timbwili hilo (litarushwa hewani kupitia Global Online TV).

 Mapaparazi wetu walimtafuta Dogo Janja kwa njia ya simu, alipopatikana alifunguka: 
“Kweli siku ile tulipomaliza shoo tu tulimuona huyo demu (Farida) anakuja kwetu. Ghafla jamaa akatokea na kuanza kugombana. Sisi tuliondoka sasa kama jamaa kamuacha mpenzi wake ni yeye mwenyewe, sisi hatukuondoka naye,” alisema Dogo Janja

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers