OMMY DIMPOZ NDANI YA MUSCAT OMANI KWA AJILI YA SHOW LEO USIKU..!! TAZAMA PICHA HAPA | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Friday, March 28, 2014

OMMY DIMPOZ NDANI YA MUSCAT OMANI KWA AJILI YA SHOW LEO USIKU..!! TAZAMA PICHA HAPA

Hit maker wa Tupogo na nyimbo nyingine kibao kama Miss Koi koi Ommy Dimpoz yupo nchini Muscat kwa ajili ya Show za kimuziki  ambapo leo siku ya Ijumaa ya tarehe 28/3/2014 atatoa Burudani kwa Mashabiki wake wa Muscat.

Unaambiwa Ommy Dimpoz ndiye staa wa  bongofleva anaetajwa kuwa wa pili kwa kupokea malipo makubwa kwenye show mbalimbali anazozifanya (milioni nane kwa show za ndani ya nchi).
Siku kadhaa baada ya kutua Tanzania akitokea Marekani na Uingereza alikokwenda kufanya showz pia, Ommy Dimpoz amekula dili jingine zuri kwa kualikwa kuimba na band yake aliyotoka nayo bongo katika party ya kampuni ya mafuta huko Muscat Oman.


Kwa siku kadhaa Ommy ambae ni miongoni mwa vijana wachache wa bongofleva wanaosifika kwa kujituma na kuwa serious na kazi, alionekana akifanya mazoezi na band yake ambayo ndio atahusika nayo mwanzo mwisho kwenye stage siku ya  leo  Ijumaa March 28 2014.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers