UTATA MTUPU...JIDE: MIMI NA GARDNER TUNAISHI KAMA KAKA NA DADA...!SOMA ZAIDI HAPA... | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Monday, March 31, 2014

UTATA MTUPU...JIDE: MIMI NA GARDNER TUNAISHI KAMA KAKA NA DADA...!SOMA ZAIDI HAPA...

Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide katika 
pozi na mume wake Gardner Habash ‘Kapteini’ .
Kumbe! Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide amefunguka kuwa yeye na mumewe, Gardner Habash ‘Kapteini’ kwa sasa wanaishi kama kaka na dada hivyo kuibua swali kivipi?

Akizungumza na Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye 
mgahawa wa staa huyo wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Jide alisema kuwa yeye na Gardner wamefikia hatua
 ya kuishi katika staili 
hiyo kutokana na mapenzi yao yaliyopitiliza.

“Gardner ananipenda sana na mimi pia vilevile nampenda sana mume wangu. Mapenzi 
yetu yamepitiliza hadi tunajiona kama vile tumezaliwa tumbo moja na ndiyo maana
 nawaambia kuwa mimi na yeye tunaishi kama kaka na dada,” alifunguka Jide.

Akiendelea kuzungumza kwa kujiamini, Jide alisema kuwa hadi simu ya mkononi 
wanatumia moja kwa ajili ya mawasiliano.
“Mimi hapa sina simu, anayo mume wangu lakini wakati mwingine nakuwa nayo 
mimi ila muda mwingi anakuwa nayo Gardner,” alimalizia Jide.

Kwa makala zaidi kuhusu usichokijua juu ya maisha ya Jide, nenda kurasa za nane na
 tisa za gazeti hili.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers