BI MWENDA KATISHAAA...KWELI UZEE MWISHO CHALINZE, MJINI KILA MTU BABY....!NI SHIDAAA...SOMA ZAIDI HAPA | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Tuesday, April 1, 2014

BI MWENDA KATISHAAA...KWELI UZEE MWISHO CHALINZE, MJINI KILA MTU BABY....!NI SHIDAAA...SOMA ZAIDI HAPA

MKONGWE kwenye sanaa ya uigizaji Bongo, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’ amefunika mbaya katika uchezaji wa muziki ambapo aliwatoa jasho hadi vijana wadogo. 

Mkongwe kwenye sanaa ya uigizaji Bongo, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’.
 Tukio hilo lililovuta hisia za wengi lilinaswa na paparazi wetu, wikiendi iliyopita kwenye sherehe ya bethdei ya Klabu ya Bongo Movie Unity, iliyofanyika wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Arcade, Mikocheni jijini Dar es Salaam. 

“Ha! Kweli nimeamini mjini hakuna mzee, uzee mwisho Chalinze, mjini kila mtu baby.
 Hebu ona Bi. Mwenda anavyocheza vizuri. Yaani anawafunika hadi vijana wadogo 
kabisa. Ni burudani sana jamani. 
“Tazama alivyopendeza, amepangilia rangi za nguo vizuri. Kweli leo ni  siku ya furaha, 
ndiyo maana ameamua kutoka tofauti na siku nyingine,” mmoja wa wasanii alisikika akiwaambia wenzake ambao walimuunga mkono.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers