CHANGAMKENI...NAFASI MPYA ZA KAZI SERIKALINI!! | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Wednesday, April 2, 2014

CHANGAMKENI...NAFASI MPYA ZA KAZI SERIKALINI!!
 TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
 
      Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
 
     Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 482 za kazi kwa waajiri mbalimbali kama ifuatavyo: MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.   i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa. iii. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili. ZAIDI CLICK LINK HII: http://www.ajira.go.tz/

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers