HABARI MPYA KUHUSU KUZAMA KWA MELI...Nahodha asema SENTENSI MOJA TU, sauti za watu walionasa zasikika...!! | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Friday, April 18, 2014

HABARI MPYA KUHUSU KUZAMA KWA MELI...Nahodha asema SENTENSI MOJA TU, sauti za watu walionasa zasikika...!!

Meli iliyozama Korea Kusini imesababisha majonzi yasiyosimulika kwa familia ya abiria 287 waliopotea na wengine walioripotiwa kufariki dunia.

Kwa mujibu wa CNN, nahodha wa meli hiyo, Lee Joon Suk amezungumza leo baada ya kuulizwa maswali mengi na waandishi wa habari na alikuwa na sentensi mbili tu.

“Naomba radhi. Sina maneno ya kusema.”
Nahodha huyo anaweza kufunguliwa kesi ya mashitaka ya uzembe uliosababisha upotevu wa maisha.

Bado haijafahamika chanzo cha meli hiyo kuzama hadi sasa huku juhudi zikiendelea kutafuta abiria waliopotea.  

Imeripotiwa kuwa kuna watu wengine wamenasa ndani ya meli hiyo na sauti zao bado zinasikika. Huku baadhi ya ndugu wameeleza kuwa wamepata SMS kutoka kwa ndugu zao walionasa.
 “Hakuna connection ya simu kwa hiyo hakuna internet. Kwa hiyo ni kutuma tu SMS. Kuna watu wachache kwenye meli, siwezi kuona kitu, kuna giza totolo. Kwa hiyo kuna wanawake na wanaume wachache. Wanawake wanapiga kelele.” CNN imeambiwa.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers