HUYU NDIO JOKATE MWEGELO,MWANADADA MWENYE UCHU WA MAFANIKIO,AJA NA BIDHAA MPYA YA NDALA!!! | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Friday, April 11, 2014

HUYU NDIO JOKATE MWEGELO,MWANADADA MWENYE UCHU WA MAFANIKIO,AJA NA BIDHAA MPYA YA NDALA!!!

                                Mwanamitindo na mtangazaji wa TV nchini, Jokate                                                                            Mwegelo.
 

Picha ya bidhaa mpya ya ndala ya Kidoti.
Mwanamitindo na mtangazaji wa TV nchini, Jokate Mwegelo amefunguka kwa kusema kuwa ameamua kufungua biashara ya ndala za brand yake ya ‘Kidoti’ kutokana na mapenzi yake ya uvaaji wa ndala kataki maisha yake ya kawaida .
“Mimi napenda kuvaa ndala, napenda kuvaa wakati nakwenda kushoot,siwezi kuvaa high hills wakati nashoot, wakati unapakwa make up unaonaee, unatengenezwa nywele, you cannot wear hills lazima uwe umevaa kitu comfortable,”.
“Kwahiyo nikaona kwamba ndala ni kitu kizuri,napenda kuvaa ndala,ni kitu easy,kuvaa rahisi halafu ni kitu ambacho watu wanakihitaji why not have ndala ambazo zina mvuto wa kipekee? Kama nilivyohaidi watu kwamba Jokate kupitia brand ya Kidoti itaanzisha bidhaa mbalimbali kukidhi mahitaji ya watu na jamii mzima.
Nashukuru kuna support kwa Kidoti yenyewe kama brand. Kwahiyo tutaendelea kutoa vitu mbalimbali vya kufurahisha. Unajua kutoa surprise ni njia moja wapo ya kufurahisha, hawakutegemea kupata kitu kuzuri lakini wamekipata. Kwahiyo ni mambo ya Kidoti hayo ni bidhaa nzuri waipokee na tutaendelea kutoa bidhaa mbalimbali.” aliongeza.
Pia Kidoti amesema kuwa bidhaa ya ndala ya Kidoti itapatikana Tanzania nzima.
“Tutasambaza Dar es salaam nzima na mikoani,kwahiyo ni kitu ambacho kipo katika mipangilio ya kusambambaza sehemu mbalimbali ili upatikanaji uwe rahisi na tunafanya jitihada za kutangaza sehemu ambazo zitakuwa zinapatikana.”
Credit:GPL

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers