INAUMA SANA....UMEME WAUA WATOTO WAWILI FAMILIA MOJA KWA PAMOJA...SOMA ZAIDI HAPA.. | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Wednesday, April 2, 2014

INAUMA SANA....UMEME WAUA WATOTO WAWILI FAMILIA MOJA KWA PAMOJA...SOMA ZAIDI HAPA..

INAUMA sana! Watoto wawili wa kiume wa familia moja, Daniel Paul (8) na mdogo wake, Emmanuel Paul (3), wamepoteza maisha wakiwa pamoja baada ya kuteketea kwa moto ndani ya nyumba. 

Miili ya watoto wawili, Daniel Paul na mdogo wake, Emmanuel Paul ikitolewa
 eneo la tukio.
 Katika tukio lililojiri majira ya saa 1:00 asubuhi, maeneo ya Mtaa wa Rufita, 
Mwanza-Road mjini hapa baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuteketea 
kwa moto huku wakiwa wamelala ndani. 
Habari za awali zilieleza kuwa chanzo cha moto huo kilidaiwa kuwa ni hitilafu 
ya umeme na kuisababishia familia hiyo majonzi makubwa ya misiba miwili kwa mpigo.

Kulia ni mama wa watoto Daniel Paul na mdogo wake, Emmanuel Paul akilia kwa uchungu.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Tabora,  OCD, Samwel Mwampashe alithitisha
 kutokea kwa tukio hilo huku akiahidi kuwa polisi watafanya uchunguzi ili kubaini 
chanzo kamili cha moto huo.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers