MAJANGAZZ BINTI WA MIAKA 16 AELEZEA MAMBO MZITO KUHUSU FREEMASON | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Tuesday, April 22, 2014

MAJANGAZZ BINTI WA MIAKA 16 AELEZEA MAMBO MZITO KUHUSU FREEMASON

Binti Fauzia akiwa amepozi nyumbani kwao maeneo ya Kigogo jijini Dar es Salaam.

Binti mmoja aliyetambulishwa kwa jina la  Fauzia (jina la mbele lipo), mwenye umri wa miaka 16, 

mkazi wa Kigogo jijini Dar amedai kutumikia nafasi ya umalkia katika imani yenye utata duniani ya 

Freemason, Uwazi linakudondoshea.

Binti huyo alikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba ili kujiunga na imani hiyo, 
alimuua mama yake mdogo kwa ajili ya kafara.

 Akizungumza na gazeti hili siku chache baada ya kuokoka akiwa nyumbani 
kwa baba yake mdogo, Kigogo, Fauzia alisema alitokea Wilaya ya 
Kahama mkoani Shinyanga alipokuwa akiishi na bibi yake.

 Alikuja Dar kwa lengo la kuendeleza mauaji ya kafara ambapo 
safari hii 
ilikuwa amuue mama yake mdogo mwingine ambaye ni mjamzito 
kwa sasa.
 Alisema kama angefanikiwa kumuua, angepandishwa cheo na kuwa malkia 
kamili katika jamii hiyo inayotafsiriwa vibaya duniani.
 ALIKOTOKEA
Fauzia alisema kuwa mara ya kwanza hakujua kama amekuwa mwanachama wa Freemason bali alichojua yeye alijiunga na uchawi wenye ushirika wa Kahama 
na Kigogo jijini Dar es Salaam ambapo mara kwa mara alikuwa akija Dar usiku 
na kufanya mambo ya kichawi kwa watu mbalimbali.
 Alisema siku moja aliambiwa lazima amtoe uhai mama yake mdogo, 
naye kwa uwezo aliokuwa nao alifanya hivyo, mama yake mdogo akafa 
kwa kuugua ghafla.
 Baada ya kifo cha mama yake mdogo, ndipo usiku mmoja bibi kizee 
mmoja 
(alimtaja jina) alimtokea katika ulimwengu wa kiroho na kumwambia 
alitakiwa aende kwenye Jiji la Lagos nchini Nigeria kwa ajili ya 
kutambulishwa rasmi na kupewa umalkia mdogo.


Baadhi ya vitu vinavyotumika kwa ajili ya kafara.
credit:blog ya mwananchi

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers